Majambazi watikisa mji wa Magugu
WATU wapatao watano wanaosadikiwa kuwa majambazi wa kutumia silaha juzi walitikisa mji wa Magugu wilayani Bahati mkoani hapa kwa risasi
baada ya kuvamia duka la Katibu wa Uchumi wa CCM wilaya ya Babati, Jafari Mchili.
Mashuhuda wa tukio hilo walilieleza gazeti hili kuwa majambazi hao wakiwa na silaha aina ya SMG walivamia duka hilo majira ya saa mbili usiku na kupora zaidi ya Sh milioni 2.5. Aidha, wamedai baada ya majambazi kufika eneo hilo la tukio, mmoja wao alianza kurusha risasi ili kuwatawanya watu waliokuwa wakipita katika maeneo hayo, huku wengine wanne wakimbana Mchili huku wakimtaka awapatie fedha.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Francis Masawe alisema watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi walirusha zaidi ya risasi kumi huku nyingi zikielekezwa katika kituo cha Polisi Magugu.
Alisema tukio hilo ambalo ni la kwanza kutokea katika mji huo mdogo unaokua kwa kasi limetokana na mwingiliano wa wageni wengi wanaoingia katika mji huo kwa lengo la kununua mchele.
Alifafanua kutokana na tukio hilo, Kamanda huyo amewataka viongozi wa kijiji hicho kushirikiana na wananchi ili kubaini dhamira za wageni wanaoingia kijijini hapo. Licha ya wito kwa wananchi pia amewaagiza askari wa jeshi hilo kituo cha Magugu kujipanga vyema kukabili watu wanaoingia kwa kigezo cha kununua mazao

No comments: