JEZI YA KESSY DILI YANGA

Shabiki wa Yanga Godlisten Chicharito akiwa amevalia uzi ambao utakuwa ukitumiwa na beki namba mbili wa timu hiyo Hassan Ramadhani Kessy
Ukiachana na Yanga kutetea ubingwa wao walioutwaa msimu uliopita, story kubwa kwa sasa
kwenye soka la bongo ni beki wa Simba Hassan Kessy kujiunga namabingwa hao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa msimu wa pili mfululizo.
Kessy tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani katika usajili wake kama mchezaji huru.
Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinasema kwamba, Kessy amechagua jezi namba 25 ambayo pia ilikua inavaliwa na Emanuel Okwi aliyesajiliwa na Yanga akitokea Simba.
Baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wameanza kuvaa jezi namba 25 ambayo ina jina la Kessy mgongoni kama ishara ya kumkubali mchezaji huyo na kumkaribisha kwenye timu yao.
Godlisten Chicharito ni miongoni mwa mashabiki wa Yanga ambao walivaa jezi namba 25 yenye jina la Kessy mgongoni wakati wa mchezo wa Mbeya City vs Yanga uliochezwa Jumanne kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Yanga kupata ushindi wa magoli 2-0.
“Hii ni jezi yangu ya pili kuvaa yenye jina la mchezaji wa Tanzania mgongoni kwangu”, anasema mnazi huyo wa Yanga nilipomtafuta na kufanya nae mahojiano mafupi baada ya kuonekana ame-shine na jezi ya Kessy.
“Nimevaa jezi ya Mrisho Ngassa namba 17 na hii ya Hassan Kessy namba 25. Kessy ni mchezaji ambaye namkubali tangu akiwa Mtibwa na Simba kwasababu anauwezo mkubwa”, aliendelea kusema Chicharito sabababu ya yeye kuvaa jezi itakayotumiwa na beki huyo namba mbili.
Baada ya kuonekana nimeivaa jezi hii nimekuwa naulizwa maswali mengi na mashabiki wengi wa Yanga kwamba inapatikana wapi, kila shabiki anataka kuipata jezi namba 25 hii inaonesha ni kiasi gani watu wanamkubali Kessy na wamempokea kwa mikono miwili.
Inatajwa kuwa, dau la milioni 40 limetumika kuinasa saini ya Kessy kujiunga na Yanga

No comments:

Powered by Blogger.