Aina 7 Za Matatizo Ya Tendo La Ndoa Kwa Jinsia Zote(Aina, Sababu & Tiba)

Kuna aina mbalimabali za matatizo ya tendo la ndoa. Leo tutazungumzia hizi chache(7):-

AINA

1. Kukosa hamu ya ngono(Hypoactive Sexual desire disorder): Hapa mtu anajikuta anakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa katika kipindi fulani cha muda mrefu tofauti na alivyozoea hapo awali. Kuna baadhi ya watu ambao wamekua na tatizo hili tangu kuzaliwa kwao.
Sababu:- huzuni, wasiwasi, kuzeeka, uchovu, mimba(baadhi hukosa hamu kabisa na baadhi hupata hamu kupita kiasi) , uzalishi pungufu wa vichocheo vya oestrogen kwa mwanamke na testosterone kwa kwa mwanaume.

2. Kutotaka kabisa(hata kusikia ngono (Sexual Aversion Disorder)
    Sababu:- huzuni, wasiwasi, kuzeeka, uchovu, mimba, uzalishi pungufu wa vichocheo vya   oestrogen kwa mwanamke na testosterone kwa kwa mwanaume.

3. Mwanaume kushindwa kusimamisha uume wake licha ya kua na hamu ya kufanya mapenzi ( Male Erectile Disorder)
Sababu:- uharibifu wa mishipa ya fahamu katika uume, mtiririko hafifu wa damu uumeni, aibu, nk

4. Mwanamke kuto toa au kutoa kiasi kidogo cha maji ya kulainisha uke (Female Sexual Arousal Disorder) Sababu::- magonjwa sugu, nk

5. Kushindwa kufikia kilele cha raha ya mapenzi ( Inhibited orgasm) licha ya kua na hamu au kusimamisha uume kwa mwanaume na kutoa maji ya ukeni kwa mwanamke.

6. Kumwaga shahawa mapema (Premature Ejuculation). Hili ni tatizo la mwanaume kumwaga shahawa mapema kabla mpenzi wake hajafika kileleni. Hakuna urefu maalumu wa muda kwa ajili ya kumwaga, lakini inashauriwa mmwago wa kwanza tokea muda uume unaingizwa isiwe chini ya dakika mbili. Kuthibitisha tatizo hili ni lazima mtu awe na historia sugu ya tatizo hili.

7. Maumivu wakati wa tendo la ndoa (Dyspareunia):- Ni tatizo zaidi kwa wanawake kuliko kwa wanaume. Sababu ni kukakamaa kwa misuli ya uke, kuzalisha maji lainishi kidogo au kutozalisha kabisa, kua na historia ya kuumizwa ama alipokua akishiriki tendo hilo kwa mara ya kwanza kwa hiari yake mwenyewe au kwa kulazimishwa(kubakwa) na hivyo kuendelea kua na mawazo hasi juu ya tendo la ngono.
 
Athari:- kukosa mtoto, usaliti katika ndoa, kutokua na amani kati ya wapenzi, nk 
Tiba:- Muone daktari kwa uchunguzi na maelekezo, muone mwanasaikolojia kwa tiba ya akili(psychotherapy), epuka pombe na sigara.

SABABU(GENERAL)
Sababu za tatizo hili ni pamoja na-
·         Sababu za kiafya:. Hizi ni pamoja na hali ya ugonjwa wa kisukari , moyo , ugonjwa wa neva(mishipa ya fahamu), upungufu wa homoni(hormonal imbalance), magonjwa sugu kama vile figo au ini kushindwa.
·          Ulevi na madawa ya kulevya. Aidha, madhara ya     baadhi ya dawa , ikiwa ni pamoja na baadhiya madawa ya unyogovu( madawa ya kulevya), inaweza kuathiri hamu na kazi ya ngono.
·  Sababu za kisaikolojia: Hizi ni pamoja na stress kama wasiwasi. Kwa mfano kijana au binti ambaye alifundishwa msikitini au kanisani kwamba tendo la ndoa ni dhami. Kwa bahati nzuri au mbaya somo hilo likamkaa hadi anapooa au kuolewa wazo hilo halimtoki na hivyo kujikuta anashindwa kupata radha au kumpa radha halisi mwenzake kwa sababu ana wasiwasi akikumbuka mafundisho ya dini yake. Yako mengi mfano experience ya kubakwa n.k

JE, MATATIZO YA KINGONO HUTIBIWA?
Tiba hutegemea sababu. Kama sababu ni  sigara, madawa ya kulevya basi dawa ni kuacha. Fika katika vituo vya afya ili kuchunguza magonjwa tajwa hapo juu. Kumbuka si kila mwenye magonjwa tuliyotaja hapo juu basi lazima awe na tatizo la ngono.

 Psycho-Sexual Disorders

No comments:

Powered by Blogger.