Kubenea aing’ang’ania UDA


Mabasi ya UDA

SAED Kubenea, Mbunge wa Ubungo ameanzisha tena mjadala wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA)
na Mradi wa Mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (UDART) bungeni jana, anaandika Happiness Lidwino.
Licha ya mapema jana Lawrance Mafuru, Msajiri wa Hazina kudai kuwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliiuzia UDA hisa kihalali, Kubenea ameendela kupinga kauli hiyo na kuongeza, UDA imeuzwa kifisadi na taratibu hazikufuatwa.
Kubenea amesema, hisa za mradi huo ziliuzwa kinyume cha sheria kutokana na tamaa ya viongozi wachache waliokuwepo madarakani wakati mradi huo ukiuzwa kwa Kampuni ya Simon Group Limited.
“Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja na kikao cha Baraza la Madiwani cha kamati ya uongozi wa Jiji la Dar es Salaam na serikali yenyewe akiwemo Msajili wa Hazina imejiridhisha kuwa, hisa za UDA ziliuzwa kinyume cha utaratibu, kwa anayejiita mwekezaji wa Kampuni ya Simon Group Ltd.
“Na kwamba, rasilimali za UDA zinazohamishika na zisizohamishika zilitawanywa katika mabenki mbalimbali kwa kuwekwa dhamana. Na mwanahisa mkuu wa hazina hakuridhishwa na uamuzi wa kuuzwa kwa UDA,” amesema Kubenea.
Anasema, mkutano mkuu wa wanahisa wa tarehe 10 Juni mwaka 2011 uliosimamiwa na Didas Massaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam katika kuidhinisha uuzaji wa UDA usiokuwa halali, serikali inajua.
Pia amesema, Bunge la Jamhuri ya Muungano linajua na kwamba, anashangazwa na hatua ya serikali kuendelea na uuzaji huo licha ya kujua ufisadi uliofanyika huko nyuma.
“Mkutano huo wa kifisadi uliitishwa na watu wanne haukukidhi akidi na ulisimamiwa na mtu mmoja   Massaburi, Robert Kisena ambaye ni Mkurugenzi wa Simon Group; Mwanasheria wa Jiji, Isack Nasoro; na Philiphs Mwakisa, Mkurugenzi wa Jiji kwenye mkutano huo ndipo ikatangazwa kuwa Simon Group imekidhi vigezo vya kuchukua UDA ambapo si kweli,” amesema Kubenea.
matangazo ya nafasi za ajira tembelea www.kibaruani.blogspot.com

No comments:

Powered by Blogger.