El Clasico: Mambo 6 ya kufahamu kuhusu mchezo huu – 1: Je hii ni Clasico ya Mwisho kwa Ronaldo? Udhaifu na ubora wa vikosi…
Zikiwa zimebaki siku 3 kuelekea mchezo wa El Clasico – Barcelona vs Real Madrid, leo nakuletea mambo matano muhimu kuelekea mchezo huu mkubwa kwa ngazi ya vilabu duniani
.
1. Timu gani inaingia kwenye El Clasico ikiwa kwenye hali nzuri ya kimchezo. Barcelona wanaingia kwenye mchezo wakiwa vizuri zaidi ya wapinzani wao – wapo kwehye rekodi ya kutofungwa katika mechi 39, hivyo wanaonekana kuwa vizuri kuwazidiLos Blancos. Lakini Barca wana wasiwasi mkubwa na wachezaji wao watatu muhimu wanaounda ‘MSN’ wanasafiri kutoka America ya Kusini kurudi Spain – uchovu unaweza kupunguza fitness yao kuelekea mchezo huu.
2. Ushindi Utamaanisha nini kwa mshindi wa El Clasico
Ikiwa Real watashinda, hali ya kujiamini itapanda katika mji mkuu wa Spain. Kutakuwepo na mazungumzo juu ya mkataba mpya kwa Zizzou na watapata kujiamini kwamba hakuna wa kuwazuia kutwaa ubingwa wa 11 wa mabingwa wa ulaya msimu huu.
Sare itawanufaisha pande zote mbili, Barca wataendelea kuwa na rekodi yao ya kutokupoteza mechi ya 40 mfululizo na pia Madrid wakinufaika kuelekea mwishoni mwa msimu wa La Liga.
3. Ni namna gani Madrid wanaweza kuiangamiza Barca?
Lakini inabidi timu pinzani ziwe na uwezo wa kukaa na mpira ili uweze kuchezea mpira kwenye nusu ya uwanja ya Barca – kikosi cha Rafa Benitez kilichodhalilishwa kwenye raundi ya kwanza ya La Liga msimu huu kilishindwa kufanikisha hilo. Madrid watahitaji kuhakikisha kutafuta mbinu ya kuzuia Sergio Busquest asiumiliki mchezo ikiwa watataka kupata matokeo chanya – wakipoteza umiliki wa sehemu ya kiungo basi hali itakuwa ngumu kwao.
4. Ni namna gani Barca wanaweza kuiangamiza Madrid?
5. Je hii ndio itakuwa Clasico ya mwisho kwa Ronaldo?
Real Madrid watatumia fedha Kwenye kipindi cha usajili kinachokuja ili kuimariaha kikosi chao chenye mapungufu kadhaa na hivyo watahitaji kuuza wachezaji ili kupata fedha za kuimarisha kikosi chao. Lakini pia wanaweza wasimuuze Ronaldo na panga likawaangukia Isco na James Rodriguez ambao wamekuwa na msimu usiovutia.
6. Je hii inaweza kuwa El Clasico ya kwanza na ya mwisho kwa kocha Zinedine Zidane.
asantee kwa news
ReplyDeleteasante kwa kuwa msomaji wa DARUBINIYAKO
Delete