Breaking News: Rais wa Zanzibar Dr Shein atangaza rasmi kufutika kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa


Akihutubia katika uzinduzi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio
uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichopata wabunge wengi isipokuwa CCM. 

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kilichopewaa ridhaa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa isipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais ama Mawaziri kutoka Upinzani. Amesema hayo ni maamuzi ya wananchi na ni lazima yaheshimiwe. Wananchi Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi.

No comments:

Powered by Blogger.