TFF: Usibet mechi ya Taifa Stars dhidi ya Chad, wamekumbushia jambo.tazama hapa
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 22 imekamilisha mazoezi yake ya mwisho pamoja na wachezaji
wake nane waliokuwa wamechelewa kuwasili jijini N’Djamena Chad na kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya March 23 kucheza mchezo wake wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON 2017).
Taifa Stars ambayo itakuwa ikiongozwa kwa mara ya kwanza katika mchezo huo na nahodha wake mpya Mbwana Samatta kwa mara ya kwanza toka apewe majukumu hayo, itacheza na wenyeji Chad katika dimba la Idriss Mahamat.
Hata hivyo shirikisho la soka Tanzania TFF limeandika na kuwakumbushia ibara ya 59 kifungu cha 11 wanafamilia wa TFF kuachana na michezo ya kubahatisha maarufu kama Betting. hivyo sio busara hata mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Chad kubet.
“To not take part in betting connected with football and do not tolerate any form of manipulation or unlawful influencing of match results”
Chanzo cha Taaifa hii: tff.or.tz
No comments: