Lowassa amshinda Magufuli

Edward Lowassa, aliyekuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Ukawa, akiwasili kwenye ukumbi wa Karimjee
EDWARD Ngoyai Lowassa, sasa anaongoza rasmi jiji la Dar es Salaam. Ni baada ya Isaya Chares Mwita, aliyekuwa mgombea wa kiti
cha umeya, kutangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho, anaandika Saed Kubenea.
Isaya aligombea nafasi hiyo, kupitia vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Lowassa, waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri, alikuwa mmoja wa wagombea urais katika uchaguzi mkuu uliyopita.
Pamoja na kwamba hakutangazwa kushinda, lakini alitoa upinzani mkali na wengi wanaamini kuwa ndiye aliyestahili kutangazwa mshindi.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, uliofanyika katika ukumbi wa Karimejee, Jumanne 22 Machi 2016, Sarah Yohona, Kaimu Mkurugenzi wa jiji alisema, Isaya alipata kura 84 kati ya 151 zilizopigwa.
Kinyang’anyiro cha uchaguzi wa umeya wa jiji kimefanyika miezi mitano baada ya kumalizika uchaguzi mkuu.
Aidha, uchaguzi wa meya wa jiji umefanyika baada ya mbinu kadhaa za chama tawala – Chama Cha Mapinduzi – kuzuia uchaguzi huo kushindwa kufanya kazi.
“Kwa matokeo haya, Lowassa ndiye aliyeibuka kidedea. Yeye ndiye atakayeongoza jiji la Dar es Salaam. Magufuli (John Pombe Magufuli, rais wa Jamhuri) atakuwa chini yake,” anasema Penina Nkya, mmoja wa viongozi wa Chadema.
Naye Omari Thabiti Kombo, diwani wa Kata ya Makurumla (CUF) amesema, “ushindi tulioupata siyo wetu. Ni wa Lowassa.”

Anasema, “…tumetimiza kile ambacho tulikuwa tunakipigania kwa muda mrefu. Leo tumetoka kifua mbele na hii ni zawadi kwa Lowassa ambaye alikuwa mgobea wetu urais.”

No comments:

Powered by Blogger.