Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeibuka na ushindi wa goli 1 dhidi ya Chad kwenye michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la Afcon mchezo uliochezwa mjini D’jamena huko Chad bao likifungwa na Mbwana Ally Samatta Mshambuliaji wa kimataifa anayekipiga kule Ubelgiji kwenye klabu ya Genk.
Stars inayonolewa na kocha mzalendo Charles Boniface Mkwasa “Master” ilifunga bao hilo dakika ya 30 kipindi cha kwanza na likadumu hadi mapumuziko na timu ziliporejea zilicheza na kutoshana nguvu hivyo stars ikabaki na ushindi huo.
Bao hilo limeisaidia Stars kuifikia Nigeria kwenye msimamo wa kundi G kwa alama 4 baada ya michezo 3 na itawasubiri Chad kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa taifa Dar es salaam
Mchezo wa mapema ulikuwa ni kati ya Benin na Sudan Kusini ambapo Benin wameshinda bao 2 kwa 1.
Michezo inayoendelea hivi sasa ni kati ya Guinea Bissau na Kenya, Kenya wakiwa nyuma kwa bao moja wakati Zambia na Congo wakiwa hawajafungana huku Libya ikiwa inaongoza bao moja dhidi ya Sao Tome.
No comments: