Mwandishi aliyetekwa Zanzibar kaongea kwa mara ya kwanza baada ya kupatikana (+Video)
Habari za kutekwa kwa mwandishi wa habari wa
idhaa ya kiswahili ya DW ya UjerumaniSalma
Said visiwani Zanzibar
zilizidi kuenea katika kila kona huku
kila mmoja akiwa hajui alipo mwandishi huyo, ila March 21 kumetoka habari njema
za kupatikana kwa mwanadishi huyo.
Salma Said amepatikana na
kuongea kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari baada ya kutekwa kwa zaidi ya
siku mbili “Nitaeleza kwa kifupi sana kwa sababu ni uhuni
na unyama niliyofanyiwa, nilitekwa wakati nipo Airport nikisubiri gari yangu
ije kunichukua, ndipo waliponichukua kwa nguvu na kupandishwa katika gari yao”
>>> Salma Said
“Jana ndio wakanirudisha nilipokuwa karibu na
kituo cha Tax cha Airport ilikuwa saa 11 alfajiri huku usoni nikiwa bado
nimefunikwa, nikajiburura hadi barabarani na kumuomba msaada mama mmoja ambae
aliniambia kaa chini mwanangu” >>> Salma
Said
Video ya Salma
Said akieleza
namna ilivyokuwa
video kwa hisani ya AYOTV
No comments: