HATIMAE SIMBA SC YAISHITAKI TFF KWA WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO NAPE NNAUYE

Hajji Manara
UONGOZI wa klabu ya Simba leo mchana umewasilisha malalamiko ya barua kwa Waziri wa Habari Utamaduni
, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye baada ya kuona Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeshindwa kusikiliza malalamiko yao.
Pamoja na kuwasilisha barua hiyo kwa Waziri mwenye dhamana, lakini pia Simba imepeleka barua hiyo kwa TFF na kumkabidhi Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Mwesigwa Selestine.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi barua hiyo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara alisema, wameamua kupeleka barua yao kwa Nnauye baada ya kuona barua zao nyingi zinazokwenda TFF zinakaliwa kimya.

Alisema dhumuni la kwenda kwa Nnauye ni kumjulisha yanayoendelea katika medani ya soka nchini.
“Tunaamini kupeleka barua kwa Nnauye, tutakuwa tumefanya kitu sahihi zaidi kwa wakati huu kwa maana Waziri anatakiwa kujua kila kitu kinachoendelea katika mchezo".
“Hatutaki tupendelewe katika masuala yeyote yale, lakini tunachotaka ni hali ambayo ambayo itakuwa sahihi kwa kila mmoja kuona mambo yanaenda kihalali zaidi na sio kama ilivyo hivi sasa” alisema Manara.

Katika hatua nyingine Manara alisema, wataendelea na msimamo wao wa kugoma kucheza michezo ya Ligi Kuu Bara, mpaka Bodi ya ligi hiyo (TPLB) itakapobadili ratiba yake ya hivi sasa.

Manara alisema, kitendo cha wao kucheza michezo 24, huku timu za Yanga na Azam, kucheza michezo 21, ni kiashiria cha upangaji wa matokeo mwishoni mwa ligi hiyo inayokwenda ukingoni.

Alisema, wanaitaka TPLB, kubadili ratiba yao ya hivi sasa ili timu za Yanga na Azam, zicheze michezo yao ndio na wao wanaweza kuingiza tena timu uwanjani.
Ratiba ambayo tunaitumia hivi sasa haiko kokote kule, haiwezekani ligi inakwenda ukingoni, lakini kuna timu zinakuwa na michezo mingi tofauti na wenzake".

No comments:

Powered by Blogger.