Jokate, Kiba Wazichapa
Wapendanao, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Kiba
‘King Kiba’,
wamedaiwa kuzichapa kavukavu ndani ya gari kisa kikiwa ni ujumbe mfupi wa
maneno (SMS), Risasi Jumamosi lina ubuyu kamili.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilitokea katikati ya wiki iliyopita maeneo ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam bila kujulikana walikuwa wakitokea wapi kwenda
wapi.
okate na Kiba awali walimwagana lakini hivi karibuni wakarudiana
baada ya familia ya Kiba, akiwemo mama yake, kuwakutanisha Februari 5, mwaka
huu kwenye Hoteli ya Slipway, Masaki jijini Dar na kumaliza tofauti zao.
Siku
hiyo ya kupatanishwa kulikuwa na hafla ya uzinduzi wa video ya Kiba iitwayo
Lupela ambayo inafanya vizuri katika soko la muziki wa Bongo Fleva nchini.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo makini, Jokate na Kiba walipishana kauli baada ya mrembo huyo
anayefanya vyema katika tasnia ya muziki, filamu na mitindo Bongo kulazimisha
kusoma ujumbe mfupi wa maneno ulioingia kwenye simu ya mpenzi wake huyo.
SIKU YA TUKIO
Chanzo
hicho kiliweka bayana kuwa wawili hao wakiwa katika mizunguko yao hivi
karibuni, walisimamisha gari lao maeneo ya Kinondoni-Biafra na ndipo walipoanza
kuzozana kwa muda kabla ya kuanza kushikana maungoni.
“Walitaitiana
kwenye gari. Wakapaki, Kiba alionekana kushuka kama anataka kumuacha Jokate
peke yake ndani ya gari, Jokate hakukubali, akashuka na yeye kumlazimisha
arudi. Mazungumzo yalisikika Jokate akihoji ni kwa nini jamaa anamkatalia
kusoma meseji iliyoingia kwenye simu yake! Ndipo timbwili liliponoga.
“Ilikuwa
mtiti wa aina yake lakini Kiba alipoona ‘nzi’ (mashuhuda) wanaanza kujaa,
akaona isiwe tabu, akarudi ndani ya gari na Jokate naye akaingia wakaondoka
zao,” kilisema chanzo hicho kilichoshuhudia timbwili zima.
MENEJA AFUNGUKA
Kabla
ya kuwatafuta wawili hao, mwanahabari wetu alimtafuta mmoja kati ya mameneja wa
Kiba aliyeomba hifadhi ya jina ambaye aliweka wazi kuwa, wawili hao walipishana
‘Kiswahili’ kutokana na SMS ambayo haikuwa mbaya isipokuwa walishindwa
kudhibiti hasira zao.
Msikie:
“Walipishana lugha baada ya Jokate kulazimisha kusoma au kuona ujumbe ulioingia
kwenye simu ya Kiba. Halafu kwani unafikiri basi ulikuwa ujumbe mbaya,
ilikuwa ni meseji yangu niliyomtumia kumpa maelekezo ya kazi lakini Jokate
akamaindi.
“Alichokosea
Kiba ni kukataa kumpa simu sasa sijui naye ana vimeo vyake au vipi lakini hapo
ndipo utata ulipoanzia. Wakavutana kwa muda lakini bahati nzuri Kiba akawa
mstaarabu, akarudi ndani ya gari kama Jokate alivyomtaka, wakamalizana na
kuendelea na safari yao,” alisema meneja huyo.
PENZI LIPO PALEPALE
Akaongeza:
“Kwa sasa wapo freshi. Si unajua mambo kama hayo kwenye mapenzi yanatokea.
Wamewekana sawa na kila kitu kipo kwenye mstari. Wamewekeana mikakati mizuri
kuhusu matumizi ya simu.”
KIBA ANASEMAJE?
Baada
ya kuzungumza na meneja huyo, mwanahabari wetu alimtafuta King Kiba kupitia
kilongalonga chake cha mkononi ambapo alipopatikana alitoa majibu tata ambayo
gazeti lilishindwa kubaini kama amekubali au amekataa.
Msikilize:
“Kwa nini kila siku mnaniuliza habari za skendo tu? Mbona hamniulizi kuhusu
muziki wangu unavyofanya vizuri kitaa au hujasikia ngoma yangu ya Lupela
inavyokamata chati? Acha mambo yako bwana.”
Akaongeza:
“Halafu, hata kama ni kweli wewe tatizo lako ni nini? Mengine ni mambo binafsi.
Haipendezi kila ninachofanya au kinachonitokea nikitangaze kwenye vyombo vya
habari. Mimi nafikiri uwe unaniuliza zaidi kuhusu kazi yangu ambayo mashabiki
ndiyo wanataka kuijua.” (akakata simu).
JOKATE HAPOKEI SIMU
Jitahada
za kumpata Jokate ili aweze kuzungumzia sakata hilo ziligonga mwamba baada ya
mrembo huyo kutopokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu chochote.
Jokate
na Kiba kwa sasa ni ‘kapo hot’ ambayo mashabiki wengi wanawaombea wafikie hatua
ya kuoana licha ya kuwa na mvutano kutoka kwa wazazi wa Jokate ambao waliwahi
kuripotiwa kutoafiki uhusiano huo.
Chanzo:
GPL
No comments: