Wolper, Dk. Fadhili Siri Yao Yavuja
Siri imevuja! Daktari wa Kitengo cha
Sayansi na Tiba Asili kilichopo
Mbezi-Afrikana, Dar, Dk. Fadhili Emily amedaiwa kumponza mwigizaji Jacqueline
Wolper kwa mpenzi wake wa sasa, Mkongo baada ya picha yake kukutwa kwenye simu
ya mwigizaji huyo.
Chanzo kilicho karibu na Wolper kimepenyeza habari kuwa Wolper
ambaye yupo nchini Afrika Kusini akijivinjari na Mkongo wake, simu yake
ilinaswa na Mkongo ikiwa na picha za zamani za msanii huyo akiwa na Dk. Fadhili
walizopiga wakiwa mkoani Mwanza, sambamba na kuona mawasiliano yanayotia shaka
kati yao.
“Huwezi amini, Wolper
kamaindiwa kinoma na Mkongo. Amegundua wana mawasiliano ya siri na mbaya zaidi
amekuta picha tata za Wolper na Dk. Fadhili walizopiga miaka ya nyuma ndipo
Mkongo akaja juu na kumtuhumu kwamba kama amehifadhi picha hizo, basi
huenda wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu,” kilisema chanzo
hicho huku kikimtumia mwandishi wetu picha hizo zilizozua ugomvi.
Baada ya kunyaka habari
hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Wolper bila mafanikio baada ya simu yake
kuita bila kupokelewa. Alipotafutwa Dk. Fadhili, alisema yeye haoni shida kuwa
na Wolper hivyo kama Mkongo amemshindwa, amuachie.
“Wolper nilimpenda na
nitaendelea kumpenda. Nilishamwambia kwamba atazunguka kote lakini mume wake wa
halali ni mimi,” alisema Dk. Fadhili.
Chanzo:GPL
No comments: