Chuchu afunguka kuhusu weupe wa mpenzi wake Ray,kumbe naye…
Chuchu
Hans ameongelea weupe wa Ray nakusema
sasa amependeza kutokana na maisha yake
kubadilika kwani zamani kwake maisha yalikuwa magumu na muda mwingi alikuwa
akitembea kwa miguu na kuhangaika kutoka kimaisha ndiyo maana alikuwa
anaonekana vile.
“Unajua mimi huwa sipendi sana watu wanapozungumzia suala hilo ila
kwa kuwa sisi ni watu maarufu inafika mahali unaamua kupotezea tu, unajua watu
wanashindwa kuelewa kuwa maisha yamebadilika na saizi sanaa ina lipa ndiyo
maana Ray Kigosi amebadilika na kutakata, unajua zamani maisha hakuwa na uwezo
sana na alikuwa anahangaika na kutoka na muda mwingi alikuwa akitembea kwa
miguu ndio maana alikuwa akionekana vile” Alisema Chuchu Hans
Kwa upande
wake Ray Kigosi alikiri kuwa sasa amebadilika na kuwa mweupe na kusema siri
kubwa ni yeye kunywa maji sana, kufanya scrub ndiyo maana amekuwa hivyo ila
hajichubui kama ambavyo watu wanasema.
No comments: