WARIOBA ATOA SIRI ZA UKAWA, AELEZA KWANINI AMEENDELEA KUBAKI CCM, SOMA HAPA

Waziri Mkuu wa zamani , Jaji Joseph Warioba na mwenzake katika wadhifa huo kwa nyakati tofauti za utawala, Fredrick Sumaye , walishindanishwa ndani ya vyama Chadema, NCCR-Mageuzi , CUF na NLD vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ili kupata jina la mmojawapo atakayeshawishiwa kuwania urais.
"Nilikataa na nikatoa sababu za kukataa. Mwisho ilinilazimu kutoa tamko hadharani kusema sitagombea na pia nikatoa sababu" anasema Jaji Warioba.
Kwa kifupi nilisema, WALE AMBAO TUMELITUMIKIA TAIFA HADI KUNG'ATUKA NI WAJIBU WETU KUBAKI HUKO TULIKO NA KUWA WASHAURI WA KIZAZI KIPYA BADALA YA KUTAFUTA MADARAKA UPYA" aliendeleza kusema Jaji Warioba.

" Mwezi Desemba mwaka jana nilipokuwa kwenye mdahalo Mwanza nilipewa gazeti ambalo lilikuwa na habari kwamba Ukawa wameniteua kuwa mgombea urais. Kwamba mimi (Warioba) na Mheshimiwa Sumaye tulishindanishwa na mimi nikawa MSHINDI.

Baada ya Mdahalo wa Mwanza nilikwenda kijijini kwangu Nyamuswa. NIKIWA PALE SUMAYE ALIPITA KUNISALIMU KITOKEA BUTIAMA, NILIMUONESHA GAZETI HILO NA WOTE WAWILI TULIAMUA KUPUUZA YALIYOANDIKWA. Lakini baada ya muda mfupi nilipata ujumbe rasmi wa UKAWA.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alitumwa kuniuliza kama nitakuwa tayari kugombea urais kama mteule wa UKAWA. Nilisema HAPANA na kumueleza sababu zangu.

NILIONGEZA KUSEMA KWAMBA HATA KAMA NINGEKUWA NA NIA HIYO NINGEJARIBU KUPITIA CHAMA CHANGU LAKINI HATA HUKO NIMEKATAA. Haukupita muda nikaletewa ujumbe mwingine. Safari hii alikuja Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA" alisema Warioba katika mahojiano yake na Raia Mwema.

Jaji Warioba aliendelea kusema " KWENYE KIPINDI CHA DAKIKA 45 KWENYE ITV NILIULIZWA KAMA UPINZANI UMEFIKIA HATUA YA KUCHUKUA UONGOZI WA NCHI. NILISEMA, HAPANA.

Kabla ya hapo nilikuwa nimetoa ushauri kwa UKAWA. Nilisema mimi ni muumini wa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo naamini itafika wakati vyama vitabadilishana madaraka. CHAMA CHA SIASA NI SERA, KUMTAFUTA MGOMBEA KUTOKA CHAMA KINGINE NI KUAJIRI MAMLUKI. MIMI NI MUUMINI WA SERA ZA CCM.

KAMA NIKIENDA UKAWA , SIYO KWA SABABU ZA KUAMINI SERA ZAKE. NITAKUWA MAMLUKI KWA LENGO TU LA KUPATA MADARAKA.

Utaratibu wa aina hiyo unaweza kudhoofisha upinzani. Akiingia kiongozi kutoka nje atabadili sera za chama, ataleta watu wake kutoka chama chake cha zamani na baadhi ya wanachama wa UKAWA watakimbia.

Niliwakumbusha jinsi NCCR-Mageuzi ilivyokuwa na nguvu lakini akadhoofika baada ya kuingia kiongozi kutoka nje. Naamini jambo kama hili linaweza kutokea kwa UKAWA na hasa kwa Chadema na hii haitakuwa kwa faida ya nchi"

No comments:

Powered by Blogger.