Wanawake walalamika kwa mke wa Lowassa

WANAWAKE wilayani Meatu mkoani Simiyu wamelalamikia kitendo cha kuuziwa
kadi za kliniki Sh 3,000, wanapokwenda kupata huduma ya kupimwa. Hali hiyo, imesababisha wajawazito wengi washindwe kuhudhuria kniliki kwa sababu ya kukosa fedha.

Wakizungumza kwa masikitiko mbele ya mke wa mgombea urais kwa wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa,mama Regina Lowassa, akina mama hao walisema wanashindwa kuanza kliniki kutokana na gharama kubwa.

Walisema baadhi ya wauguzi katika hospitali za serikali mkoani Simiyu, wamekuwa wakidai fdeha ili wawapime . Mmoja wa akina mama hao, Fatuma Selmani alisema kuna baadhi ya akina mama amepoteza maisha kutokana na kutokuhudhuria kliniki, kwa sababu wengi wao wanajifungulia majumbani Walisema kero nyingen, walisema wamekuwa wakizuiwa na mabwana shamba wasilime kilimo cha mseto kwa kuchanganya mahindi na pamba.

Alisema kutokana na ukame, wanalazimika kulima kilimo cha kuchanganya mazao ili waweze kujikinga na njaa Naye Teresia Edward mkazi wa kijiji cha Miringi,alisema wamechoshwa na uonevu huo.

Kwa upande wake, mama Regina alisema kuna haja ya Serikali kusikia kilio cha akina mama hao, kwani kwa wajawazito ni muhimu ndiyo maana kadi hutolewa bure.

Kuhusu elimu, alisema kila mtoto atasoma bure kwa sababu Ukawa wamedhamiria kuondoa tatizo la watoto kukosa shule. “Wanawake wenzangu naomba mwaka huu msiniangushe Oktoba 25, mpeni kura za ndiyo Lowassa ili apate ridhaa ya kuongoza,”alisema

No comments:

Powered by Blogger.