Urais 2015: Warioba amfananisha Magufuli na Nyerere
Aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kwamba Mgombea Urais wa CCM Dr. John Pombe Magufuli ni mtu muadilifu, Mchapakazi na Asiyekuwa na tamaa hivyo anazikaribia sifa za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika juzi mjini Bunda, Warioba alisema Dr. Magufuli ndiye anayestahili kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kati ya wagombea nane kutoka vyama mbalimbali vilivosimamisha wagombea kwani mpaka kufika kwake hapo hakujatokana na fedha wala harufu ya fedha yeyote.
Alidai kuwa Vyama vya upinzani vilitakiwa kusimamisha wagombea wao wenyewe bila kuazima kutoka Chama cha Mapinduzi CCM jambo ambalo linawaondolea sifa za siasa zao za upinzani wa kweli nchini.

No comments: