Pete ya Uchumba ya mtesa Wolper
Stori: Mwandishi wetu
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Walper ‘Wolper’ amejikuta akitoa machozi ya furaha baada ya kuvalishwa pete ya uchumba na kijana anayedaiwa kuwa ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
....Wakifurahia kwa pamoja.
Wolper ameitundika picha yake katika mtandao wa kijamii wa Instagram, akiwa na kijana huyo anayetajwa kuwa mwenye ‘hela mbaya’ akionyesha kidole chake kikiwa na pete hiyo ya madini ya Tanzanite ‘white gold na Diamond’, lakini akatoa machozi kwa kukumbuka uchumba wake wa awali na Dallas ulivyoyeyuka.Akionesha pete aliyovalishwa na mchumba wake huyo.
“Nimelia kwa sababu awali nilikuwa na furaha kama sasa, lakini nikajikuta nabakia peke yangu, ninaomba Mungu anisaidie iwe kweli, maana nimemsubiri mchumba kwa muda mrefu sana,” alisema muigizaji huyo, akitaja thamani ya pete hiyo kuwa ni dola 3000, ambazo ni sawa na shilingi milioni sita na ushee za Kibongo.
Aidha, licha ya kuvalishwa pete hiyo, mrembo huyo pia alizawadiwa mkufu wenye thamani ya dola 1600 sawa na mil3.5
No comments: