Nimeupenda Ukauzu wa Dr. Maghufuli Kutokumshirikisha Mkewe Katika Kampeni za Kusaka Urais

Magufuli
Tumlizoea, kwenye chaguzi nyingi, wagombea kuambatana na wenza
wao, kwenye campaign, hii hali imezusha maswali kibao, hasa kwa marafiki zangu wa UKAWA, wamediriki hadi kunitania wakisema Magufuli hana mke, hatutaki Rais bachelor, lakini niliwajibu kuwa ana mke na watoto, ikumbukwe magufuli sio mtu wa kujivuna, Mungu amsaidie, pia anajua anachofanya ni kwa manufaa ya taifa, hata watoto wake wanasoma shule hizi hizi za St Kayumba, hivyo sio mtu wa kujiweka matawi ya juu, Magufuli ana hofu ya mungu kama hutaki kajinyonge. Dkt. Magufuli ni mmoja ya mawaziri wanaoogopwa sana kwa misimamo hata na Rais mwenyewe kwa jambo analoliamini analifanya kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu.

Amemuekeza Kanali Kinana kuwa moja hatapenda kuiona familia yake ikishiriki katika kampeni za urais kwani sitaki familia yangu kujihusisha au kujinasibisha na urais wa nchi.

Nataka nikapambane kufuta hili lililojengeka kwa watoto wa vigogo kubebwa kwenye nafasi za uongozi hata ajira na kuwaacha watoto wa watanzania maskini wakiwa mitaani eti kwa sababu hawana wa kuwashika mikono haki ya Mungu hili nitapambana nalo ili chama hiki kiwe cha wote na nchi hii iwe ya wote.

Hivyo mke wangu naomba aachwe akafundishe,wanangu waendelee na mambo yao na hata ndugu zangu. Jukumu lao kubwa ni kuniombea kwa Mungu ili nikawatumikie watanzania kwa moyo wa dhati bila kiburi na majivuno.

#hapakazitu

No comments:

Powered by Blogger.