Nay wa mitego alizwa na mrembo
AMEPIGWA! Ndivyo vijana wa mjini wanavyosema kuakisi tukio la staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuibiwa na mrembo pochi iliyokuwa na zaidi ya shilingi laki 8, vitambulisho vyake mbalimbali kikiwemo cha kupigia kura, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.
Tukio hilo la kumzidi ujanja Nay lilitokea Septemba 7, mwaka huu maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo msanii huyo alikuwa kwenye moja ya gereji bubu akiwekewa ‘tinted’ ndipo alipodondosha pochi hiyo alipokuwa amekaa ndani ya gari kisha kuibiwa.
“Yeye (Nay) alikuwa amekaa kwenye gari wakati mafundi wakiendelea kuweka tinted, sasa akanyanyua miguu na kuweka kwenye dashboard huku akiongea na simu. Pochi yake ikaanguka, sasa nafikiri aliiona lakini kwa kuwa alikuwa bize na simu hakutaka kuiokota ndipo mrembo mmoja aliyekuwa anauza juisi akaja kumdai hela kwani Nay alikunywa juisi muda mchache uliopita.
“Nay akaingiza mkono mfuko wa mbele, akampa hela yake yule mrembo alipoona pochi imedondoka, akaichukua kiaina bila Nay kushtukia mchezo, akasepa zake. Nay alikuja kushtuka baadaye na kugundua kapigwa ndipo mafundi walipomwambia huenda ni yule mrembo wa juisi,” kilisema chanzo chetu.
Akizungumzia tukio hilo, Nay alikiri kuibiwa fedha taslim zaidi ya shilingi laki 8 na kusema tukio hilo lilikuwa la kusikitisha lakini anamshukuru Mungu vitambulisho vyake vimepatikana japo fedha hakuzipata.
“Siku ya tukio nilimsaka yule mrembo bila mafanikio lakini kesho yake wale mafundi wangu waliniambia wameikuta pochi imetelekezwa katika gereji yao ikiwa na vitambulisho lakini fedha zimeibiwa zote,” alisema Nay wa Mitego.
No comments: