Mgonjwa alilia matibabu
NASIKITISHA, Said Ndangaye Mwilu (57), mkazi wa Kimara Baruti, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam na mwenyeji wa Kilwa, Kijiji cha Kipatima, anaishi katika hali ya mateso makubwa baada ya sehemu ya mwili kuanzia kiunoni hadi miguu kupooza na kuibuka tundu kwenye kalio, magonjwa ambayo amedumu nayo kwa muda mwaka mzima.Said Ndangaye Mwilu
akiugulia.Akizungumza na gazeti hili, mzee huyo amesema amekosa huduma za kimatibabu baada ya kukosa shilingi milioni sita kwa ajili upasuaji.Akisimulia zaidi mzee Mwilu alisema kutokana na hali yake ya ugonjwa huo amekata tamaa kwani amehangaika katika hospitali mbalimbali jijini kwa ajili ya kupata matibabu lakini tatizo linazidi kuwa kubwa na hali yake kifedha ni hovyo kwani hana kitu chochote cha kumwingizia kipato.“Zinatakiwa shilingi milioni sita ili nifanyiwe upasuaji na niweze kupona lakini sina,” alisema alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wetu wodi ya Kibasila namba 13 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Akielezea tatizo lilivyoanza alisema ilikuwa mwanzoni mwa 2014 lakini ilipofika Oktoba 2014 tatizo lilishika kasi kwa maana ya kupooza mwili kuanzia sehemu ya kiunoni hadi miguuni.“Uchunguzi umeonesha kuwa kuna baadhi ya pingili katika mgongo wangu zimelika kisha kupishana na ndiyo chanzo kikubwa cha kupooza na kulazwa kitandani kwa miezi kadhaa sasa,” alisema.Akaongeza kuwa, alikwenda hospitali mbalimbali kutibiwa bila mafanikio ndipo aliamua kwenda Muhimbili kufanyiwa vipimo ikabainika kupooza kwake kumetokana na pingili za mgongoni kuachana.“Kinachoniumiza zaidi ni mwanangu Felex Lazaro anayesoma Imam Ecademic yupo nyumbani kwa kukosa ada, naomba Watanzania wanisaidie kwani naweza kufa kwa sababu sina fedha,” alisema Mwilu.Wakati tunaenda mtamboni tulipata taarifa kutoka kwa mwanaye aliyejitambulisha kwa jina la Allen Mwilu kuwa mgonjwa huyo amemhamishia katika Hospitali ya Dk. Kairuki jijini Dar.Aliyeguswa na habari hii anaweza kuwasilina na mgonjwa huyo kwa namba 0658 154027
No comments: