Mama Zari amaliza ubishi
MAMA mkwe wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye pia ni mama mzazi wa mzazi mwenza wa staa huyo, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’, Halima Hassan amempigia chapuo msanii huyo kwa kumpa baraka zote kwamba ndiye baba mzazi wa mtoto Latiffah ‘Tiffa’.
Kwa mujibu wa ‘yuda’ wa familia ya Diamond (aliomba hifadhi ya jina), mama Zari alitua jijini Dar Jumatatu iliyopita akitokea Kampala bila kufafanua kama alikuja sambamba na Zari au la kwa vile hivi karibuni, mrembo huyo aliripotiwa kuitwa kwao kisa kikiwa ni mtoto huyo.
MAMA ALIKUWA NA SHAKA
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, awali bibi Tiffah alikuwa na shaka juu ya ukweli kuhusu baba wa mjukuu wake huyo kufuatia minong’ono kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kwamba, Tiffah ni mtoto wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga.
Aidha, mnyetishaji huyo akasema: “Mbali na madai kwamba mtoto ni wa Ivan, mama Zari alichanganyikiwa zaidi kuambiwa kwamba, kuna mwanaume mwigine ambaye ni rafiki wa karibu wa Ivan, King Lawrence naye kaibuka na kusema mtoto ni wake na yuko tayari hata apimwe kipimo cha kinasaba.”
CHA KWANZA BAADA YA KUFIKA DAR
Ikaendelea kuelezwa kuwa, bibi huyo baada ya kutua Dar, alimchukua Zari na kukaa naye peke yake kwa muda wa dakika thelathini akimkazia sura mtoto huyo huku akimpekua sehemu mbalimbali za mwili.
“Unajua huyo mama ni mgumu sana kuamini mambo juujuu. Hapo awali alijua kuwa huenda Tiffah kweli ni mtoto Ivan. Hata alipotua Bongo, alipofika nyumbani, kabla hajapumzika aliomba kwanza amuone mjukuu wake.
“Lakini alipomuona, hapohapo aliachia kicheko huku akisema, ‘kweli ni mtoto wa Diamond kutokana na kufanana kwa mambo mengi. Kwa sasa ametoa baraka zake zote kwa ‘wanandoa’ hao na ameumaliza ubishi wa muda mrefu wa mtoto ni wa nani,” alisema ‘kikulacho’ huyo.

DIAMOND ANASEMAJE?
Mpashaji mwingine kutoka ndani ya familia hiyo ya Diamond, aliliambia gazeti hili kuwa, baba Tiffah ambaye yuko nchini Nigeria, baada ya kusikia baraka kutoka kwa mama mkwe wake amefurahi sana.
“Diamond amefurahi sana. Msimamo wa awali wa mama Zari juu ya kuwa mtoto ni wa Ivan, ulikuwa ukimkosesha amani kabisa. Kwa sasa ana baraka zote za mkwewe,” alisema mwanafamilia huyo.
Ilizidi kudaiwa kuwa, mama Zari alisema kwa mara ya kwanza alimwona Diamond nchini Uganda ambapo nyota huyo alikwenda kwa ajili ya shoo moja.
“Tangu pale, mama Zari alimkubali Diamond. Aliukubali uhusiano wake na binti yake. Lakini pia alipenda penzi lao kwa vile mwanaye alishaumizwa na wanaume huko nyuma,” kilisema chanzo bila kumtaja mwanaume aliyemuumiza Zari.
TUGEUKE NYUMA KIDOGO
Hapo awali, siku chache baada ya Zari kujifungua, ziliibuka tuhuma, shutuma na madai mazito, kwa kile kilichoitwa ‘Diamond kauziwa mbuzi kwenye gunia’ kwani mtoto huyo ni wa Ivan, mume wa zamani wa Zari, jambo ambalo kijana huyo kutoka Tandale lilimkosesha amani na furaha licha ya kujitutumua kuwa, anaamini mtoto ni wake.

Diamond alitumia ushahidi wa maneno ya Zari mwenyewe alipomhakikishia kwamba hakuna baba mwingine wa mtoto huyo aliye gumzo Bongo na Uganda
No comments: