Haya ndio anayo enda kujifunza Dimond Nigeria?

Nyuma ya safari za mara kwa mara za Mbongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ za nchini Nigeria, kumeibuka madai mazito kuwa, anapokwenda huko hufundishwa mbinu za uchawi ili kukubalika duniani kama mastaa wa huko, Risasi Jumatano limenyetishwa.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja, Diamond anafundishwa uchawi na Wanigeria kwani ndiyo taswira ya sanaa yao inavyoakisi duniani ambapo ukiwa nchi nyingine ukauliza kuhusu nchi hiyo, meseji kubwa katika sanaa yao ni utamaduni wao hasa suala la ndumba.
Ilidaiwa kwamba, mila na desturi za nchi hiyo zimeelekezwa zaidi katika mambo hayo hivyo hata wasanii wake maarufu wanadaiwa kuegemea humo.Kuhusu hilo, bila kutaja majina, ilidaiwa kwamba, kuna baadhi ya wasanii waliotenga vyumba maalum ambako wameweka vitu vyao vinavyohusiana na mambo hayo na huwa wanaviamini kuwa vinawasaidia kuwika kwenye ulimwengu wa sanaa.
DIAMOND ANAHUSISHWAJE?
Kutokana na ukaribu wake na baadhi ya mastaa wa Nigeria, Diamond anatajwa kuelekezwa kwa ‘mafundi’ wa huko.
“Unajua wanasema kila mgeni lazima awe na mwenyeji. Kwa hiyo jamaa zake wa kule ndiyo humwelekeza walipo mafundi,” kilisema chanzo kimoja.
TUZO ZATAJWA
Ilisemekana kwamba, kutokana na suala hilo ndiyo maana Diamond anazidi kupasua anga kwenye ulimwengu wa muziki akiipaisha vyema Bongo Fleva na kuzoa tuzo kibao za kitaifa na kimataifa na kupata shavu la kufanya kazi na wasanii wakubwa wa Marekani kama Shaffer Chimere Smith ‘Ne-Yo’.
Madai hayo yalikwenda mbali zaidi na kunyetisha kuwa ndiyo maana Diamond ameshiriki katika kolabo nyingi na mastaa hao kwani hupata nafasi ya kuhudhuria hata ibada zao za asili, hivyo ndiyo sababu ya mwendelezo wake wa kuwa karibu na jamaa hao ambao baadhi ni waumini wa ibada hizo za asili.
HE! KUMBE ZARI ANA UKARIBU NA WANIGERIA!
Ikadaiwa kwamba, hata utajiri alionao na mafanikio ya mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ chimbuko lake ni hukohuko kwani naye ana ukaribu mkubwa na mastaa wa Nigeria na amekuwa akifanya nao biashara mbalimbali lakini bila kuwekwa wazi masuala ya ndumba.
Mastaa wa Nigeria ‘Naija’ wanaotajwa kuwa ndiyo huwa wenyeji wa Diamond na wengine ameshafanya nao kazi ni pamoja na Peter na Paul Okoye (P-Square), David Adedeji Adeleke ‘Davido’, Kingsley Chinweike Okonkwo ‘KCEE’, Yemi Alade, Tiwa Savege, Oladapo Daniel Oyebanjo ‘D’Banj’ na wengineo ambapo mara tu anapotua Nigeria humpokea na kumpa kampani hadi anaporudi Bongo.
DIAMOND ASAKWA, YUPO NIGERIA
Kufuatia madai hayo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Diamond kwa njia ya simu ambapo lilielezwa kuwa yupo nchini Nigeria ambako ana ‘projekti’ mpya na baadhi ya mastaa hao wakiwemo D’Banj na Omotola Jalade Ekeinde.
Risasi Mchanganyiko liliamua kumtumia meseji kupitia Mtandao wa WhatsApp na kumuuliza maswali mawili.
Kwanza lilimuuliza kuhusu madai hayo ya kufundishwa ndumba Nigeria, pia lilimuuliza kuhusu madai ya mtangazaji Loveness Malinzi ‘Diva’ kusisitiza kuwa, kufuatia ugomvi wake na Diamond kwa kumtukana ndani ya studio wiki iliyopita, hawezi kumsamehe, anamburuza kortini.
Baada ya muda, Diamond alijibu swali moja tu kati ya hayo mawili. Nalo ni la Diva akisema:
“Mimi nasoma kwako kwamba atanipeleka kortini. Mimi sijapata barua yoyote ile ya kuitwa huko kortini.”
AMEWAHI KUTAMKA 
Hata hivyo, mara kadhaa, Diamond yeye amekuwa akikanusha vikali juu ya ishu hiyo ya kutumia uchawi kwenye sanaa akisema kuwa hakuna kitu kama hicho na huwa anamwamini Mungu na anaswali swala tano.
“Mimi namtegemea sana Mungu kwenye kazi zangu na bidii katika kazi ndiyo maana hata nalala studio kwa sababu nataka nifike mbali kwenye hii kazi hivyo nashangaa sana watu kuzusha kwamba natumia uchawi,” alisema Diamond siku kadhaa zilizopita.
-Chanzo: GP

No comments:

Powered by Blogger.