Hii ndio orodha mpya ya majina ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mkopo chuo kikuu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (HESLB) imetoa orodha ya Awamu ya Tatu ya wanafunzi 7,901 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 29,578.
Katika Awamu ya Kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo na Awamu ya Pili wanafunzi 11,481.
Orodha hiyo ya Awamu ya Tatu inapatikana HAPA  au unaweza kutembelea kwenye tovuti ya Bodi (HESLB) (www.heslb.go.tz).
Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bil 427.54 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na tayari Serikali imeshatoa shilingi bil 147.06 kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.

No comments:

Powered by Blogger.