MTOTO WA HAYATI Sehemu Ya 3
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3xZNbCRFlAqh0NrYpCUIMlok4Qc9Z-yo61D2jj9V-TtztTHSpvkizJgI_9rfc1xGPj5l-uRe4CuROr8BsW9kyuWgaCse8_X-pbF2kPpw8t301kWCbzWlMz3A2Ex5M-XMw_7Smg70SNOMv/s640/MTOTO+WA+HAYATI.jpg)
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓
Sasa nikiwa naendelea kupewa matibabu ya goti, mara mamkubwa
alimuuliza dokta kua
"dokta, choo chenu kipo wapi"
"aaaa choo kipo kulia ukishapita hio kordo hapo mbele
yake kuna vyoo"
"ok asante"
Nilimwambia mama kua tuondoke zetu
"mama, twende kwa baba"
"hebu subiri utibiwe we mtoto"
"mama mi staki matibabu tena"
Mara dokta akadakia juu kwa juu
"dogo tulia namalizia kukufunga bendeji tu"
Yaani kile kitendo cha mamkubwa kuondoka roho yangu ilikua
ikidunda mno,
"sheby kwani una nini lakini"
"mamkubwa anaenda wapi"
"si anaenda msalani, kwani hujasikia hapo akiulizia
uwani"
"mamaaa we twende bwana"
"nitakuchapa sasa pumbavu wewe, kikiwa kikubwa hiki
utamsumbua nani? Hebu tulia mwehu wewe"
Nilitulia lakini sikua na amani kabisa juu ya mamkubwa
kuenda uwani,
ENDELEA............
Basi dokta aliendelea kunifunga bendeji huku, akiipakia dawa
ili mchubuko ule usilete shida, kweli familia yangu ilikua ikinipenda sana,
kana kwamba yaani mchubuko kidogo tu tayari napewa matibabu, na hapo ni mama,
kama ngekua ni baba ungekuta hata kutibiwa nisingetibiwa hapa, maana karibia
magonjwa yangu yote hua napelekwa nje ya mkoa wa arusha, yaani sitibiwi arusha,
basi zoezi liliendelea mpaka mamkubwa akarudi kutoka uwani huku
akimuuliza dokta
"mmmhh dokta bado tu"
"aaaaaa mama si unajua watoto hawa tunaenda nao
taratibu mno"
"ni kweli baba"
Mara ghafla nesi kaja resi huku akimuita dokta kwa uharaka
zaidi
"dokta dokta njoo haraka yule mgonjwa kazidiwa"
Dokta hakutaka kuuliza ni mgonjwa gani aliezidiwa, badala
yake aliniacha na kukimbilia huko, ila sisi hatukushtuka sana maana hapo ililua
ni hospitalini, hivyo sio kila mgonjwa ni wako tu,
"vinauma"
Mama yangu aliniuliza huku akipashika shika kwa kuangalia
kama kuna maumivu ambayo naweza kuyasikia,
"haviumi, mi niliwaambia hakuna shida lakini mkanileta
tu"
"mwanangu, kidonda ni kidonda tu hata kama kiwe kidogo
kiasi gani"
"mmnhh sawa"
Mara dokta alirudi huku akiwa mnyonge mnyonge kiasi,
"poleni sana jamani"
"poleni? Pole ya nini dokta"
Mama ndio alimuuliza dokta huku wote tukimtumbulia macho
dokta huyo, ili atueleze hio pole anampa nani
"aaaa kiukweli, mume wako ametutoka mama"
Nilimuona mama nae akalegea pale pale, huku mamkubwa
akiangua kilio, Mimi nilitoka na kuelekea kwenye hio wodi ambayo baba yangu
alikua kalazwa, Sikuamini macho yangu baada ya kukuta baba yangu akiwa
keshafunikwa shuka jeupe, lililomfunika mpaka kwenye macho, Sikuweza kuvumilia
juu ya lile, nami nilianza kulia kwa uchungu mkubwa huku mamkubwa akija huku na
yeye akilia, Nilimlilia baba yangu huku nikigala gala hapo chini kwa uchungu wa
kumpoteza baba yangu mzazi, Mamkubwa alikuja kuniamsha huku akinibembeleza kwa
maana mimi ndio niliokua nalia kuliko wote, nilimuona baba yangu akichukuliwa
na kupelekwa kwenye chumba cha watu walio na hali hio, yaani MOCHWALI yaani
sikua nikiamini macho yangu kwa kile nilichokua nikikiona juu ya hali ile,
Baada ya hapo nilianza tena kumtafuta mama angu maana toka
alivyolegea pale ofisini kwa dokta, sikujua kaeleka wapi tena,
"dokta dokta, mama yangu yupo wapi"
"usijali, we tulia na mamkubwa wako maana mama yako nae
hali yake sio nzuri"
"naomba nikamuone mama yangu dokta"
Nilikua nalia kwa uchungu mno huku nikimsumbua dokta
anipeleke alipo mama, yangu ili nimuone,
"mama yako, yupo wodi namba 9 palee"
Niliwahi kwenda kumuona mama ambae na yeye hali yake ilikua
mbaya baada ya kusikia kua baba au mumewe amepoteza maisha, na hapo hapo mama
yangu akalegea akiwa kakaa kwenye kiti, nilimkuta mama yangu nae kalazwa
tena huku madripu yakiwa yamemzunguka kitandani kwake,
"mamaaaaaaaaaaa, ooohhhhh mama, mamaaaa baba hayupo
tena mama, uuuuuwiiiiiiiii"
"sheby mwanangu nyamaza, mama ako anaumwa muache
kwanza"
"sitaki niache nikae na mama angu"
"twende nyumbani ukale"
"sitaki hata kula...... Iiiiiiiiiiiiiiiii
oooooooooooojjujj uuuuuuuuuuuuuuuuhhhhhh nnnnnnnnnnhhhhhh
uuuuuuuuuuuuuuuuhhhhhh uu uuuwiiiiiii"
"sheby baba, unampigia mama kelele"
"sitaki niacheee"
Mamkubwa alikua akiniamsha kwa nguvu eti nitoke hapo wodini
lakini sikua tayari kutoka,
Nilitoka tena na kuelekea mochwali kumuangalia tena baba
yangu, Nilizuiwa kuingia mochwali, nilirudi tena kule alipokua mama yangu na
kuendelea kukaa nae karibu maana najua kilichomuua baba yangu, ila hata
nikisema sintosikilizwa na mtu yeyote hivyo bora nitulie tu,
Baada ya siku mbili kupita, hali ya mama ilikua nzuri,
na alikubaliana na matokea ya kifo cha baba, tulikodi gari la kusafirishia
maiti, huku sisi tukiwa ndani ya gari yetu ndogo aina ya vx nyeusi mayai mayai
hivi, tulikua tukielekea tanga kumzika baba, kiukweli nilikua nina huzuni sana
juu ya baba yangu,............
Tulifika kijijini hapo maeneo ya pongwe kunako makazi ya
mzee, yaani ndio nyumbani, Basi kama kawaida maandalizi yaliandaliwa kwa ajili
ya mazishi, kiukweli sikua na raha kabisa.....
Baada ya siku mbili kupita, tulishamzika baba katika nyumba
yake ya milele, Nilikua nina uchungu mkubwa sana juu ya kifo cha baba yangu,.......
Sikutaka kulala nyumbani maana kesho yake ilikua tunarudi arusha, aisee
huezi amini nilienda makaburi usiku kukaa kwenye kaburi la baba huku nikilia
sana, yaani sikuridhika kabisa kwa kifo cha baba yangu, nilijikuta usingizi
ulinipitia pale pale makaburini, maana nilitarajia ifikapo saa 3 usiku nirudi
nyumbani, lakini usingizi ulinipitia pale pale makaburini, kwakua ilikua ni
usiku na nisingeweza kutembea na giza hivyo niliingia kwenye kichaka cha karibu
kisha nikawa nimejilaza, maana tanga kuna joto kwa wakati ule,.... Kiukweli
mimi ni muoga sana ila kwa kifo cha baba yangu, aiseee huezi amini uoga
uliniisha kabisa
Sasa nikiwa pale kichakani, ghafla niliona watu kwa mbaali,
tena wakiwa wamevaa kanzu, lakini tembea yao hawakua wakitembea kama kawaida,
yaani walikua kama wamekaa afu wanakuja huku nilipo, nikaona bora niende
nao nyumbani, maana huenda nikawa nimepata kampani ya kunisindikiza, hivyo
nilikua nawasubiria wafiki karibu ili niwasimamishe, basi na mimi nikaamka na
kusimama ili niwafuate, lakini kabla sijaanza kuwafwata, ghafla niliona wengine
kwa upande mwingine tofauti na wale wa mwanzo, nikajua daaaahh kampani imekua
kubwa, maana ilikua ni mishale ya saa 6 hivi kwenda saa 7 usiku,.....
Niliona nikojoe kabisa ili nikianza safari nianze kabisa......
Nilitamani wafike haraka ili niniunge nao kwenda nyumbani, maana
wanaonekana ni mashehe wanatoka kwenye shughuli. Hivyo nilitoka ndani ya
kichaka kile na kuanza kuwapungia mkono japo ilikua ni usiku wa kutisha......
Itaendelea
No comments: