Lema alivyokamatwa Dom-Arusha
Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alikamatwa kwa mara ya pili mfululizo ndani ya wiki hii na kuhojiwa na polisi kwa madai ya kutoa lugha za uchochezi.
Juzi, Lema alikamatwa kwenye viwanja vya Bunge na kusafirishwa usiku huo na polisi hadi wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma ambako walimkabidhi kwa Polisi wa Mkoa wa Arusha.
Hiyo ni mara ya pili, kwani kabla ya hapo akiwa Arusha alikamatwa na polisi na kuhojiwa kwa madai ya kutoa lugha ya uchochezi. Kabla ya kukamatwa juzi akiwa bungeni, taarifa zilizagaa na yeye alijua kuwa angekamatwa na kupelekwa Arusha, lakini alisema yuko tayari kufa kwa kuwatetea wanyonge hivyo haoni shida kwa lolote linalotokea mbele yake.
Lema alichangia hotuba ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2017/18 na baada ya hapo mbunge huyo alitoka ukumbini akiwa ameongozana na mmoja wa wabunge kutoka Chadema, huku akitumia lango ‘C’ ambalo ni la wageni.
No comments: