BREAKING NEWS: LEMA KWELI KIBOKO AWANYOOSHA VIKALI MAJAJI WA KESI YAKE KWA MAAMUZI MAZITO ALIYOFANYA MAHAKAMANI
Hali hiyo ilitokana na mbunge huyo kutofikishwa mahakamani kutoka mahabusu kwa sababu ambazo hazikufahamika. Kesi hiyo ilikuwa ianze kusikilizwa kwa Lema na mke wake, kusomewa maelezo ya awali.
Kukosekana kwa mbunge huyo kuonekana mahakamani, kulimlazimu Hakimu MkaziMfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Augustino Rwezile, kutoa amri ya kutolewa hati ya kumtoa mahabusu na kumfikisha mahakamani ili kesi ianze kusikilizwa.
Hata hivyo, tangu amri hiyo itolewe saa nne asubuhi, hadi saa saba mchana, mshitakiwa hakufikishwa mahakamani hapo, licha ya mke wake kuwapo.
Rwezile alimtaka Wakili wa Serikali kueleza sababu za kushindwa kumfikisha Lema mahakamani wakati chombo hicho kimeshatoa amri. Wakili wa Serikali, Fotunatus Mhalila, alidai mshitakiwa ameshindwa kufikishwa mahakamani kutokana na sababu zisizozuilika.
Hata hivyo alidai kwa sababu upelelezi umekamilika, anaomba mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa hoja za awali.
Majibu hayo yalipingwa vikali na Wakili wa Utetezi, John Mallya, ambaye alitaka ufahamu sababu za kutomfikisha Lema, alizodai hazikuweza kuzuilika ni zipi, na ni vyema zikatajwa mahakamani.
“Mheshimiwa Hakimu hizo sababu zisizoweza kuzuilika ni zipi, Wakili wa seriali atueleze, tujue kama siyo amedharau mahakama licha ya kutakiwa umleta mshitakiwa,” alidai.
Baada ya hoja hizo kutolewa, Hakimu Rwezile alisisitiza hati ya kumtoa mahabusu itolewe ili mshtakiwa afikishwe mahakamani leo katika kesi hiyo, ambayo itasikilizwa hoja za awali.
Lema na mke wake Neema, walisomewa mashtaka kuwa kati ya Agosti 20, mwaka huu, ndani ya jiji la Arusha, walimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani Gambo wenye lugha ya matusi,huku wakijua ni kosa kisheria.
Ilidaiwa kuwa ujumbe huo ulituma kutoka 0764150747 namba 0756551918 kwenda namba 0766-757575 uliokuwa ukidai, “Karibu, tutakuthibiti kama Uarabuni wanavyothibiti mashoga.
” Wakati huo huo, waandishi wa habari jana walipata wakati mgumu kutekeleza majukumu yao, kutokana na askari wa Jeshi la Polisi wakishirikiana na wa Magereza kuwazuia kuingia kwenye chumba cha Mahakama na kufukuzwa nje ya uzio wa mahakama kwa madai kuwa ni maagizo ya mahakama.
Hatua hiyo iliwafanya waandishi kuandamana hadi kwa Hakimu Rwezile, ambaye alikana mahakama kutoa amri yoyote ya kuzuia waandishi kufanya kazi yao.
“Nawaomba msamaha na poleni kwa usumbufu mliopata. Ila nitaongea naaskari wa pande zote mbili ili tueleweshane, maana mnatekelezamajukumu yenu ya kikazi na kama barua tunawapatia za utambulisho na vitambulisho mnavyo kwa nini mzuiwe.
No comments: