ZITTO AMTOLEA UVIVU RAIS KABILA WA KONGO NA JPM WA TANZANIA KUHUSU MALIPO YA $50 KWA WANANCHI
Kupitia ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe amesema ...."Rais Kabila Na Rais Magufuli ondoeni visa kwa Wananchi wetu wanaoingia kwenye Nchi zetu za Jamhuri ya KiDemokrasia ya Kongo Na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kurahisisha Biashara miongoni mwa Nchi zetu.
Hivi sasa raia ya Kongo anayeingia Tanzania analipa $50 za visa. Vile vile raia wa Tanznaia anayeingia Kongo. Hiki ni kikwazo kikubwa sana cha Biashara hasa Mpakani mkoani Kigoma, Katavi Na Rukwa".
No comments: