Yanga waikacha Dar sasa kuamia Zanzibar

Baada ya serikali kupitia kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo Mh. Nape Nnauye kupiga marufuku timu za Simba na Yanga kyumia uwanja wa taifa kwa muda usiojulikana, klabu ya Yanga imekiandikia barua Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar kuomba kuutumia uwanja wa Amaan kama uwanja wao wa nyumbani.

Barua hiyo iliyoandikwa na Katibu wa Yanga Baraka Deuedit, inalengo la kuomba kuutumia uwanja wa Aamaan kwa mashindano mbalimbali ambayo inashiriki ikiwemo ligi kuu Tanzania bara (Vodacom Premier League).

Mh. Nnauye alizipiga marufuku Simba na Yanga kuutumia uwanja wa taifa ambao unamilikiwa na serikali kufuatia uharibifu uliofanywa na mashabiki wa timu hizo kwa kung’oa mageti manne pamoja na kung’oa viti wakati wa mchezo wa Jumamosi October 1.

Lakini hata hivyo, kanuni za ligi zinaibana Yanga kwasababu, moja ya kanuni hizo inavitaka vilabu vinavyobadili uwanja, kuchagua uwanja ambao upo katika mji au mkoa jirani na mkoa wa timu husika ndani ya Tanzania bara ilimradi uwanja huo uwe na sifa zinazokubalika na uthibitishwe au uidhinishwe na TFF.

Soma kanuni zinazoelekeza timu kubadili uwanja uwanja wake wa nyumbani…


No comments:

Powered by Blogger.