Tundu Lissu afunguka hakuna anaye taka kumjaribu Rais Magufuli. Mahabusu sio kuzuri niulizeni mimi

Leo mchana, Jumanee Agosti 9, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefnya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ili kutoa taarifa kwa umma kuhusu taarifa za vitisho wanazokuwa wakizipata kutoka serikalini.

Mwanasheria Mkuu wa wa chama hicho ambaye pia ni  Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe.  Tundu Antipas Lissu amesema hakuna mtu kutoka Chadema anayetaka kumjaribu mtukufu Rais na wala hakuna anayetaka kukamatwa na polisi  kwa sababu mahabusu sio pazuri.

“Tunachotaka kukifanya ni ambacho kipo katika katiba, mikutano na maandamano ya kisiasa kwakuwa ni halali. Kama kufanya hivyo Rais Magufuli anafikiri tunamjaribu hayo ni mawazo yake” Amesema Tundu Lissu.

No comments:

Powered by Blogger.