LISU NOMA APANGUA HOJA ZA SERIKALI NA KUPATA DHAMANA. SOMA HAPA ILIVYO KUWA

FATILIA VIZURI KESI YA LISU ILIVYO KUWA LEO MAHAKANI KISUTU........

YALIYOJIRI MAHAKAMANI KISUTU: LISSU APATA DHAMANA:

Tayari timu ya vichwa 13, vikiongozwa na KIBATALA vilivyobobea katika mambo ya SHERIA, imefanya yao, sasa wameelekea chumba cha dharula

Updates:

Kuna ubishi wa kitoto unaendelea...
Upande wa serikali wanapinga Wakili Kibatala kuwa sehemu ya jopo la mawakili wa Lissu

Updates:

Mahakama imerejea baada ya kusimama kwa nusu saa..

Hoja ya mawakili wa serikali kuwa Kibatala asiwe wakili wa Lisu badala yake awe shahidi upande wa jamhuri inaanza kubishaniwa....

Mabishano ya vifungu ni mkali ,wao wakijenga hoja kuwa kibatala awe shahidi wa jamuhuri asiwe wakili wa lisu

Hakimu: Kibatala punguza kingereza kidogo tumekubaliana lugha ni kiswahili...

Kibatala akomae na kiingereza nahisi hawa mawakili wa serikali kinawapiga chenga sana

Mawakili wa Serikali wanatoa macho kama mafundi SAA! Vifungu anavyovitaja Kibatala nafikiri hawavisoma

Kibatala anapangua hoja kwa vifungu mpaka Hakimu anafurahi

Nitadili nao kisheria mpaka wanijue mimi ninani ,hakuna mwenye uwezo wakunizuia nisimwakilishe mteja wangu

Mahakama haiendeshwi kwa maneno ya kusikia,wewe kuwa mwanasheria mkuu wa Serikali haimaanishi utanizidi kisheri, Nataka mjue kuwa hamna mamlaka yoyote ya kisheria hatakama ni Mawakili wa Serikali humu ndani wote ni sawa!

Hakimu amekataa hoja ya mawakili wa serikali yakutaka Mh Peter Kibatala asimtetee Lissu na badala yake awe shahidi wa Jamhuri...

Hivyo Kibatala ataendelea kuwa Wakili wa Mh. Lissu.

Kwa historia ya ufanyaji kazi wa mahakama zetu nchini,
Mahakama hazikuwa kufanya kazi hadi muda huu 19:00:55HRS
Lakini leo historia inaandikwa kwa kesi ya Wakili Msomi na Mwanasheria Mkuu wa Chadema Mh. Tundu Andipas Lisu, Mahakama ya Kisutu kesi inaendelea...

Updates:

Hati ya kuzuia dhamana imewasilishwa kwa hakimu ikitoka kwa Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Ilala ambae kaapa mshitakiwa asipewe dhamana kwasababu

Kiapo kina sema endapo mshitakiwa akipewa dhamana atarudia tena kosa na kutakuwa na uingiliwaji wa upelelezi unaoendelea

Katika hati hiyo imeeleza namna ambavyo mshitakiwa akiwa nje kwa dhamana ataathiri upelelezi hivyo tunaomba dhamana ifungiwe kwa wiki mbili.

Kibatala: Mheshimiwa Hakimu hiyo huruma ya upande wa jamuhuri juu ya mteja wangu imeanza lini?? Kama shauri hili hutaweza kuliamua twende Mahakama Kuu ifanye maamuzi ni hayo tu Mheshimiwa hakimu

Hakimu: Mawakili wa Serikali fanyeni haraka nyie ndio mmenichelewesha na lazima Leo niandike ruling

Upande wa utetezi unajiandaa kupangua hoja hiyo.......

UPDATES.!

Upande wa Jamhuri umemaliza kuwasilisha, sasa ni upande wa mshtakiwa.

KIBATALA: Mheshimiwa Hakimu sisi tunaomba mteja wetu apewe dhamana. (Mawakili wa Jamhuri wanaingilia kati. Wanapinga Kibatala kumtetea Lissu maana watamtumia kama shahidi baadae).

Lissu anasimama.....

LISSU: Mheshimiwa Hakimu, Wakili Kibatala ni wakili wangu, na hakuna sheria inayomzuia kunitetea. Lakini kama upande wa Jamhuri hautaki anitetee basi nitajitetea mwenyewe...

Hakimu anamruhusu Lissu kujitetea.

Lissu kaomba hati ya kiapo na vitabu vya sheria. Mawakili wa Serikali wote wamesimama na wanapinga Lissu kujitetea. Hakimu anawataka wakae chini. Lissu kaambiwa aendelee....

Mheshimiwa hakimu naomba nijibu hoja za kupinga dhamana zilizotolewa
Na upande wa Serikali

Kiapo ambacho kipo mbele yako hakina Tarehe ya kiapo chenyewe na hakuna anuani

Hivyo kiapo hiki si halali

Kifungu cha 8 cha sheria za viapo kina sema kwamba kila kamishna wa viapo atataja kwa Ukweli mahali kiapo hicho kilipotolewa na Tarehe ya kiapo hicho

Mheshimiwa Mahakama zetu za juu katika kesi mbali mbali wamesma kamishna wa viapo lazima aoneshe anuani na lazima aandike Tarehe

Naomba kiapo hiki usingalie kabisa

Mheshimiwa aya ya 7 na ya8 ya kiapo imeeleza namna ambavyo mm ninyimwe dhamana kwa ushahidi ambao Mahakama yako haijui

Wanataka niende magereza na Kiapo chenyewe kinasema ni disclosed kwasababu za kuungaunga naomba usikubali Mheshimiwa Hakimu

Maamuzi ya Mahakama za Africa kusini ni za ushawishi tu hazikufungi Mheshimiwa Hakimu hapo hakuna kitu kisheria

Inawezekana kabisa sheria za Africa kusini ni za 1976 kipindi cha Ubaguzi wa rangi haziendani kabisa hivyo Mheshimiwa hizo zisikupe shida

Mheshimiwa kwa sheria za Tanzania imeeleza kwa kina sababu za kininyima dhamana,na katika sheria hiyo hakuna mahali imeeleza kufanya makosa mahali pamoja ni kigezo cha kunyimwa dhamana

Niliopewa kisheria kwasababu ya unprove allegations

BREAKING NEWS. SAA 19:20 JIONI.

TUNDU LISSU APEWA DHAMANA.

Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mheshimiwa Kamanda Tundu Lissu amepewa dhamana Muda huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam.........

Mungu mkubwa..... Tulianza na MUNGU, Tuko na MUNGU na tutamaliza na MUNGU.

No comments:

Powered by Blogger.