EPL: Arsenal vs Liverpool, nani kuuanza vyema msimu jumapili hii

Ligi kuu ya England imerejea tena baada ya kuisubiri kwa takribani miezi 3, na katika wikiendi ya kwanza tu, tunabahatika kushuhudia mchezo wa timu kubwa: Arsenal vs Liverpool. Kuelekea pambano hilo tuangalie takwimu na rekodi mbalimbali kabla refa Michael Oliver hajapuliza kipenga ndani ya dimba la Emirates. 
Hali za timu zote

Wachezaji wote waliosajiliwa na Arsenal,  Granit Xhaka na Rob Holding wanategemewa kuanza dhidi ya Liverpool lakini mlinzi wao Per Mertesacker, Gabriel na Carl Jenkinson wote wana majeruhi.  
Danny Welbeck pia atakosekana kwa sababu ya majeruhi, wakati Laurent Koscielny na Olivier Giroud bado hawana ufiti wa kuanza. 

Liverpool wanaweza kumkosa Daniel Sturridge na James Milner kwa sababu ya majeruhi ya paja na kisigino. 
Sadio Mane, Georginio Wijnaldum nq Joel Matip huenda wakaanza au mupata nafasi baadae. 

Takwimu za Mchezo

Arsenal wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya 10 ya hivi karibuni ya EPL na kombe la ligi  (W5, D4, L1).Ushindi wa Liverpool pekee katika mechi 20 zilizopita za ugenini dhidi ya Arsenal katika mashindano yote ulikuja baada ya kipindi cha miaka 15, katika mchezo wa Premier League mnamo August 2011 (W1, D8, L11).Kuna rekodi ya Premier League ya uwepo wa hat tricks 5 katika mechi ya wababe hawa wawili.  Mechi za Premier League za wababe hawa zimezalisha magoli 16 katika katika ya 90 au zaidi.  Liverpool wamefunga 9 na Arsenal 7. 

Arsenal

The Gunners wamepoteza mechi 2 kati ya 3 za mwisho za nyumbani katika mchezo wa ufunguzi wa msimu.  Walimaliza msimu wa 2015-16 wakiwa na rekodi bora ya kutokufungwa katika mechi 10 mfululizo katika ligi.  Wakishinda 5 na sare 5. Arsenal walimaliza nafasi ya pili msimu uliopita,  nafasi ya juu zaidi tangu mwaka 2005. Hata hivyo walikuwa ndio timu ya kwanza tangu Manchester United msimu wa 2003-04 kushindwa kutwaa ubingwa baada ya kuongoza ligi mpaka kufikia January. Olivier Giroud amefunga magoli 4 katika mechi 4 za mwisho za ligi vs Liverpool.  

Liverpool

Liverpool wamemaliza nje ya Top 5 katika misimu 6 kati ya 7 iliyopita.   Wamekuwa na rekodi nzuri chini ya Jurgen Klopp, wakiwa na wastani wa kupata point 1.6 kwa mchezo – walikuwa na wastani wa 1.5 katika mechi 8 za mwanzo mwa msimu kabla ya kuteuliwa kwa kocha huyo Mjerumani.  Liverpool wamefunga magoli 41 ya EPL ndani ya mwaka 2016. Roberto Firmino amefunga magoli 9 na kutengeneza manne katika mechi 15 za premiere league kwa mwaka 2016, yakiwemo mawili vs Gunners mnamo January.  

No comments:

Powered by Blogger.