Done Deal: RASMI POGBA ASAINI MANCHESTER UNITED

Manchester United wamekamilisha rasmi usajili wa miaka mitano wa Paul Pogba kutoka Juventus ya Italia kwa ada ya paundi milioni 100.

Pogba (23), ambaye alikuwa akihusishwa na United kwa muda mrefu, sasa amekuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka ulimwenguni, akimpiku Gareth Bale ambaye alisajiliwa na Real Madrid kutoka Tottenham mwaka 2013.

“Manchester United wanayo furaha kubwa kutangaza rasmi kwamba Paul Pogba amekamilisha uhamisho wake kutoka Juventus ya Italy,” klabu ilitoa taarifa kupitia tovuti yao

“Paul amesaini mkataba wa miaka mitano, huku kukiwa na option ya kuongeza mmoja.”

Inaarifiwa kwamba Pogba atavuta kiasi cha paundi mil 104 kabla ya kodi kwa miaka yote mitano atakayokuwa hapo.

Awali kabla ya kuondoka klabuni hapo, Pogba alicheza michezo saba tu na hata hivyo hivyo hakufanikiwa kumaliza dakika tisini kwenye ligi ya England wakati huo United iko chini ya Sir Alex Ferguson.

Kwa usajili huo wa Pogba, United sasa inakuwa imesajili wachezaji wanne muhimu Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan, Eric Bailly na Pogba mwenyewe

No comments:

Powered by Blogger.