Dk Kigwangalla na Dr Mwaka ni chuki binafsi?

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangalla amesema hana ugomvi binafs na tabibu, Juma Mwaka wala hajawahi kusoma naye kidato cha tano na sita Sekondari ya Kigoma kama inavyoelezwa.

Dk Kigwangalla alisema hayo jana alipozugumza na gazeti hili. Alisema hajawahi kuwa na urafiki na tabibu Mwaka kama ambavyo mitandao ya kijamii na magazeti yanavyoripoti.

Desemba 14, mwaka jana, Dk Kigwangalla alitembelea Kituo cha Tiba Asili cha Foreplan Clinic kinachomilikiwa na Mwaka, ambacho kilifungiwa na Serikali na kubaini mambo kadhaa yanayodaiwa kufanywa kinyume cha sheria. Mojawapo ni la kujitangaza kwa kujiita daktari kinyume na Sheria

No comments:

Powered by Blogger.