SHEMEJI ANANITAKA,JANA KAJA CHUMBANI.. NAOGOPA KUMWAMBIA DADA, NI MKOROFI NA PIA HATANIAMINI..NIFANYEJE

Kaka, nakupongeza sana kwa kuwa na blog nzuri, inatusaidia sana, mungu akubariki, mimi nina shida, ninaishi na dada yangu ambae tumechangia baba, ila mama zetu ni tofauti, baba yetu alikufa, ndugu wakamuomba dada anichukuwe anisomeshe kozi yoyote ile,

Nikahamia kwa dada , sasa toka nimefika hapa, shemeji yangu ananifata sana, ananitaka kimapenzi, kwa nguvu na kunitishia kuwa anaenisomesha ni yeye na sio dada yangu, hivyo nimkubalie tufanye siri, Ananifata hadi chuoni, ananinyima raha kabisa, mchana ananifata anitoe luch, yani ah! ananisumbuwa sana na namshangaa amekuwa na wivu hata kwangu, hataki nipigiwe simu na mwanaume, anapekuwa simu yangu, sana, nimejitahidi kumkwepa lakini wapi

Dada yangu ana asili ya kiburi sana, ni mkali kias kwamba hata mama yake anamuogopa, na yeye ndie ameolewa na mwenye uwezo kidogo, hivyo wote wanamtegemea yeye, sasa naogopa kumwambia tabia za mumewe,  maana najua kabisa hatoniamini, na atanifukuza nitashindwa kusoma,,

Ninawaza niwaambie watu wazima wamwambie dada, lakini nina uhakika 100% dada hatoniamini, maana hupenda kusemasema kuwa, akiskia mtu yuko na mumewe, yeye hatadili na mumewe atadili na yule anaemchukulia mumewe, sasa mimi nahofia kukosa masomo yangu, maan shemeji mwenyewe anamjua mkewe alivyo, na kuna siku aliniambia unafikiri ukimwambia dada yako ndio atanifanya nini? Acha ujinga wewe, hutamani maisha ya dada yako, wewe nipe uone ntakavyokupa maisha mazuri,

nakosa raha kabisa, nisaidieni kwa ushauri wadau

nifanye nini mimi??? Kaka usiirushe email yangu please!!!

2 comments:

  1. DADA POLE KUNA BAATHI YA MIANAUME HAINA MAANA KABISA

    ReplyDelete
  2. Balaa jamaa anahaki ya kupambana

    ReplyDelete

Powered by Blogger.