PICHA 12: MATUKIO YALIYOJIRI NJE YA UWANJA FAINALI YA NDONDO CUP 2016

Mashindano ya Ndondo Cup yananogeshwa na mashabiki wake kwa asilimia kubwa, ubunifu na aina yao ya ushangiliaji umekuwa ukiwavutia hata wale ambao hawana mazoea ya kuangalia mpira.

Sasa Julai 30 kulikuwa na balaa nje ya uwanja kati ya pande mbili za ushangiliaji wakati wa pambano la fainali kati ya Temeke Market dhidi ya Kauzu FC. Kila upande ulikuwa umejipanga kuhakikisha unaufunika upande mwingine na hapo ndipo burudani yenyewe ilipo.

Chief wa Kauzu kama kawaida yake aliingia uwanjani kivingine, safari hii alikuwa ndani ya chungu lakini akakutana na Market nao wakiwa wamejipanga vizuri pale walipotinga uwanjani wakiwa na mtumbi wao.

Angalia picha uone matukio mbalimbali yaliojiri nje ya uwanja wakati Temeke Market ikiisambaratisha Kauzu FC kwa bao 3-1 na kunyanyua ndoo ya Sports Extra Ndondo Cup 2016.

No comments:

Powered by Blogger.