KAULI YA PADRI BAADA YA KUSHIRIKI FUTARI MSIKITINI DAR






hata katika imani waislamu na wakristo wana amini kuwa Mungu ni mmoja na ipo siku ya hesabu ipo, na hivyo kitendo cha kuonana katika imani moja ni moja ya sababu kubwa ya kushirikiano” Alisema

Katika kuendeleza hilo jana jioni Sheikh Jalala aliamua kuandaa futari ya pamoja katika msikiti wa Masjid Alghadiir uliopo Kigogo Dar es salaam na kuialika kamati ya AMANI ya mkoa huo,  Kamati inayojumuisha viongozi wa dini mbalimbali ndani ya mkoa wa huo, ambayo iko chini ya uongozi wa mwenyekiti wake Samahat Sheikh Alhady Mussa Salim (sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam).

Sala ya jamaa ilisaliwa Masjid Alghadiir, Sala hiyo iliongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Samahat Sheikh Alhadi Mussa, na baada ya hapo futari ikaliwa kwa pamoja ambapo Padri John Solomoni baada ya kupata mwaliko wa futari alijiandaa kwa kufunga siku nzima.. 


No comments:

Powered by Blogger.