UBINGWA WANUKIA JANGWANI, YANGA INAHITAJI POINTI HIZI KUTWAA KOMBE
Yanga imebakiza pointi nne pekee ili itangaze ubingwa wa Vodacom Tanzania bara kwa msimu huu wa 2015-2016
.
Vijana wa Jangwani wamefanikiwa kuvuna ushindi wa magoli 3-1 kwenye mchezo wao dhidi ya Stand United ya mkoani Shinyanga kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
Mshambulizi wa Yanga Donald Ngoma ametupia mbao mbili katika ushindi huo akifunga goli la kwanza dakika ya pili baada ya kuanza kwa mipindi cha kwanza kabla ya kutumbukia tena kwenye nyavu dakika ya 44 ikiwa ni dakika moja kabla ya mapumziko.
Mrundi Amis Tambwe akaunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Simon Msuva kuipa Yanga bao la tatu huku likiwa ni bao lake la 20 kwenye ligi na kumzidi kwa bao moja mshambuliaji wa Simba Hamisi Kiiza ambaye wanachuana kuwania kiatu cha ufungaji bora.
Stand United walipata goli la kwa mkwaju wa penati uliokwamishwa wavuni na Elius Maguri dakika ya 81 kipindi cha pili baada ya Thabani Kamusoko kumuangusha mchezaji wa Stand kwenye box. Bao hilo la Maguri ni la 12 kwenye ligi msimu huu.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga indelee kujichimbia kwenye kilele cha ligi huku ikihitaji pointi nne tu kutetea ubingwa wake. Yanga sasa imefikisha pointi 68, kama itapata pointi nne itafikisha jumla ya pointi 72 ambazo haziwezi kufikiwa na Azam wala Simba hata kama zitashinda michezo yao yote minne iliyosalia ambazo.
Azam inapointi 59, ikishinda mechi zake zote nne itafikisha jumla ya pointi 71, Simba pia ina pointi 58 na ikishinda mechi zake zote zote itafikisha pointi 70 na kuiacha Yanga ikitwaa taji hilo kwa mara nyingine tena.
No comments: