Sare ya 2-2 ya Tottenham vs Chelsea usiku wa jumatatu iliipa ubingwa wa kihistoria Leicester  City. Ubingwa huu umeleta
hamu ya kujua mambo mengi kuihusu Leicester na mimi nitajaribu kukuletea makala fupi fupi kuhusiana na mabingwa hawa England.
1. Sare ya Spurs jana imewapa Leicester ubingwa wa kwanza wa EPL, na kuingia katika vitabu vya kumbukumbu vya mabingwa ambao hawakuwahi hata kufikiriwa katika michezo yote ulimwenguni.
Msimu uliopita, Mbwa mwitu hawa waliepuka kushuka daraja kwa kushinda mechi 7 kati ya 9 za mwisho za EPL baada ya kukaa mwishoni mwa msimamo wa ligi kwa muda mrefu wa msimu. Hili ndio kombe la kwanza la Leicester katika ngazi ya juu kabisa ya soka la England..
2. Leicester City walitumia kiasi cha dola million 80 kusajili kikosi chao chote, upungufu wa $500m wa fedha walizotumia Manchester City kwa kikosi chake cha sasa. City walilipa kiasi cha $84 million kumsajili kiungo Kevin De Bruyne peke yake kwenye dirisha la usajili la kiangazi lilopita.
3. Moja ya stori za kuvutia kuhusiana na Leicester City ni wachezaji wake: mfungaji bora wao Jamie Vardy alikuwa akicheza ligi ya daraja la 5 miaka minne iliyopita. Riyad Mahrez amekuwa mchezaji bora wa EPL na kuweka rekodi ya kuwa muafrika wa kwanza kushinda tuzo hiyo. Claudio Ranieri ameshinda ubingwa wake wa kwanza wa ligi ya juu baada ya miaka 28 ya kufundisha soka.
Ukimuondoa Robert Huth hakuna mchezaji mwingine wa Leicester aliyewahi kushinda ubingwa wa EPL.
4. Timu pekee ambazo zimewahi kubeba wa England japo kwa mara moja ni  Nottingham Forest msimu wa 1977-78. Leicester wanaungana na Derby County (1971-72), Leeds United (1968-69) na Ipswich Town (1961-62) kama timu pekee kubeba ubingwa kwa mara moja tu katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.
5. Leicester imekuwa klabu ya 24 kushinda ubingwa wa England, na hii wao ndio waliomaliza vizuri ligi kuliko mwingine yoyote. Foxes walimaliza wakiwa washindi wa pili msimu wa 1928-29, mshindi wa tatu msimu wa 1927-28 na mshindi wa nne  1962-63.
6. Tangu Blackburn waliposhinda ubingwa  Premier League msimu 1994-95, Leicester ndio timu pekee mbali na  Arsenal, Chelsea, Man City na Man United.
7. Leicester walimaliza nafasi ya 14 msimu wa 2014-15 season. Mwaka huu wamepanda kwa nafasi 13 juu, rekodi ya kuvutia zaidi tangu Nottingham Forest waliposhinda ubingwa wa ligi daraja la kwanza msimu wa 1977-78 baada ya kupanda daraja msimu wa nyuma yake. Na katika mabingwa 115 waliopita katika EPL nane kati yao walimaliza chini ya nafasi ya 14 katika misimu wa nyuma yake.

No comments:

Powered by Blogger.