NINI HATMA YA YANGA KWA KUNDI HILI?

IMG_201605145_043419
Draw ya kupanga makundi mawili ya timu zitakazo chuana kuwania kufuzu hatua ya nusu
fainali ya kombe la shirikisho Afrika imekamilika na kila timu imeshajua itachuana na klabu gani katika hatua hiyo ya nane bora.
Mabingwa wa Tanzania bara klabu ya Yanga imepangwa Group A ambapo itachuana na TP Mazembe (Congo DR), MO Bejaia (Ageria) na Medeama (Ghana).
Mo Bejaia ni timu pekee kutoka Kaskazini mwa Afrika huku timu tatu zikitoka katika maeneo mengine tofauti ya bara la Afrika.
Group B lina klabu za Kawkab Athletic, Futh Union Sports (Morocco), Etoile du Sahel (Tunisia) pamoja na Ahly Tripoli (Libya).
Kundi B linazikutanisha timu zote zinazotoka ukanda wa Kaskazini mwa Afrika (timu kutoka mataifa ya Kiarabu) na hiyo imetokana na timu tano za ukanda huo kufuzu hatua nane bora kati ya nane.
Makundi Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup)
Yanga-conf
CAF pia imepanga makundi ya klabu bingwa barani Afrika kwenye makundi mawili kila kundi likiwa na timu nne.
Kundi A la klabu bingwa Afrika linajumuisha timu za Zesco United(Zambia), Al Ahly SC (Misri), Asec Mimossas (Ivory Coast) na Wydad AC (Morocco)
Wakati Kundi B likiwa na timu za Enyimba FC (Nigeria), Zamalek (Misri) na Mamelodi Sunddowns (Afrika Kusini)
Makundi Klabu bingwa Africa (CAF Champions League)
Yanga-conf 1

No comments:

Powered by Blogger.