MTOTO WA MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA ASAJILIWA VILLARREAL

Akram-Afif
 Kinda wa kitanzania Akram Afif mwenye uraia wa Qatar amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Qatar kusajiliwa na klabu ya Hispania.

Mtoto huyo wa mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba SC Hassan Afif amesajiliwa na Villarreal huku akionekana kuwa kuwa na kipaji cha hali ya juu kutoka taifa hilo la Mashariki ya Kati ambacho kitaisaidia klabu hiyo ya La Liga katika miaka michache ijayo.
Kijana uyo ambaye amezaliwa na kukulia mtaa wa Gerezani maeneo ya Kidongo chekundu jijini Dar es Salaam na kusoma shule zote za awali Tanzania, msimu huu alikuwa Ubeligiji akiitumikia klabu ya Eupen.
Afif ni zao la Aspire Academy inayomilikiwa na klabu ya Al-Sadd ambayo Raul Gonzalez aliitumikia kwa miaka miwili huku star wa Barca Xavi Hernández akiendelea kufurahia maisha yake ya soka.
Wale waliomfatilia kwa karibu mchezaji huyo mwenye miaka 19, wamekiri kwamba Afif anauwezo mkubwa wa kufanikiwa na miamba hiyo ya soka la Hispania na barani Ulaya. Mbali na kuwavutia ma-scout wa Villarreal, nyota huyo amevitoa udenda vilabu vingine vingi vya Hispania pamoja na klabu nyingine kama Porto na Zenit.
Afif hatakuwa na tatizo la lugha kwasababu tayari anauwezo wa kuzungumza Kispaniola kwani aliwahi kucheza kwenye academies za vilabu vya Villarreal na Sevilla kabla ya kuelekea Eupen kucheza ligi daraja la pili.
Katika kipindi alichocheza Kehrwegstadion, Afif alicheza mechi 17 na kufanikiwa kufunga magoli 6 kwenye ligi.
Tayari ameshafanya mazoezi na kikosi cha taifa cha Qatar na alifanikiwa kufunga goli kwenye ushindi wa magoli 15-0 dhidi ya Bhutan wakati timu hizo zilipokutana September 3, mwaka jana kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018.

No comments:

Powered by Blogger.