MESSI AMPONZA DOGO WA AFGHANISTAN
Unamkumbuka yule mtoto wa miaka mitano wa Kiafghanistani Murtaza Ahmadi aliyepata umaarufu mkubwa duniani
baada ya picha zake kusambaa mitandaoni zikimuonesha akiwa amevaa mfuko wa rambo (plastiki) uliotengenezwa na kufanana na Jezi za timu ya taifa ya Argentina huku ukiwa na jina la Lionel Messi?
Walimwengu hawana maana!
Sasa taarifa ziko hivi Murtaza Ahmadi ametoroka huko nyumbani kwao katika jimbo la Ghazni, Afghanistani akiambatana na wazazi wake na kwenda kuishi Quetta,Pakistani baada ya kuanza kupokea vitisho vya kuuawa.
Sasa taarifa ziko hivi Murtaza Ahmadi ametoroka huko nyumbani kwao katika jimbo la Ghazni, Afghanistani akiambatana na wazazi wake na kwenda kuishi Quetta,Pakistani baada ya kuanza kupokea vitisho vya kuuawa.
Baba mzazi wa Murtaza aitwaye, Arif, ameliambia The Daily Telegraph kuwa tangu Murtaza awe maarufu duniani yeye na familia yake wamekuwa wakipokea vitisho vingi toka kwa makundi mbalimbali ya kigaidi, waharifu na wababe wa kivita wa Afghanistani.
“Nina hofu Murtaza anaweza akatekwa na hata kuuawa. Tumeamua kukimbilia Pakistani kwa ajili ya usalama wake na wetu kwani tumekuwa tukipokea vitisho vya kila namna”, alimaliza Arif.
Miezi minne iliyopita jina la Murtaza Ahmadi liligonga vichwa vya habari vya mitandao mbalimbali dunia na hata kumfikia Lionel Messi mwenyewe.
Katika kuonesha kuwa na yeye ameguswa na upendo wa Murtaza juu yake Messi alimtumia mtoto huyo jezi yake halisi huku akiweka ahadi ya kukutana nae siku moja
matangazo ya ajira tembelea kibaruani.blogspot.com
,
No comments: