Maalim Seif Kikaangoni LEO.....Polisi Wamtaka Aripoti Makao Makuu ya Polisi Kwa Ajili ya Kuhojiwa
Baada
ya Jeshi la Polisi Zanzibar kuahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa Chama cha
Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, hatimaye hatua hiyo sasa
imeelekea kutekelezwa.
Taarifa
rasmi ya jeshi hilo visiwani Zanzibar, imemtaka Maalim Seif afike
katika Ofisi za Makao Makuu ya Polisi, Ziwani mjini hapa leo saa 4.00
asubuhi.
Mkurugenzi
wa Habari, Uenezi na Uhusiano kwa Umma wa CUF, Salim Bimani
alithibitisha Maalim Seif kupokea barua hiyo jana wakati akiwa njiani
kuelekea Dunga, Wilaya ya Kati Unguja, akiendelea na ziara yake katika
majimbo ya Unguja.
“Ni kweli Maalim amepokea taarifa hiyo na ametakiwa afike Ziwani (mjini hapa) kesho (leo) saa nne asubuhi,” alisema Bimani
Bimani
aliongeza kuwa hatua hiyo ya sasa imekuja baada ya jeshi hilo
kuahirisha hatua ya wito wa kumhoji Maalim Seif, Ijumaa iliyopita.
Barua
hiyo ya kuahirisha iliyosainiwa na Msangi kwa niaba ya Kamishna wa
Polisi Zanzibar Mei 26, yenye kumbukumbu namba PHQ/ Z/C.5/4/4/TEMP/34
kwenda kwa Maalim Seif ilikuwa na kichwa cha habari ‘Kuahirisha
mahojiano’.
“Tafadhali
rejea barua yangu PHQ/Z/C.5/4/4/TEMP 26 ya tarehe 22/5/2016 ambapo
tulikuita hapa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa mahojiano maalumu ya
masuala mbalimbali yanayohusiana na Ulinzi na Usalama wa Visiwa hivi,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo ya Msangi.
Kadhalika, barua hiyo ya kuahirisha mahojiano hayo ilisema:
“Tutakujulisha mapema siku ile iliyosainiwa na DCP Salum ya mahojiano itakayofuata mara baada ya kukamilisha taratibu.”
Msangi
alithibitisha wito huo wa leo baada ya hatua ya awali, kumtaka kiongozi
huyo awasili mbele yao kwa mahojiano kama ambavyo walimuahidi awali.
No comments: