Rais Magufuli amteua Hamphrey Polepole kuwa mkuu wa wilaya
Baadhi ya wilaya ziliachwa wazi na
Wakuu wa Wilaya baada ya kuteuliwa katika nafasi zingine
za uongozi,
April 18 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe
Magufuli amemteua Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.
Polepole anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Kamishna Msadizi
mwandamizi wa polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Uteuzi wa Hamphrey Polepole umeanza leo tarehe 18
Aprili, 2016.
No comments: