MTANGAZAJI WA CLOUDS FM GERALD HANDO AFUNGUKA KUHUSIANA NA KUACHANA CLOUDS MEDIA GROUP


Kufuatia Sintofhamu ya Watangazaji wa Clouds Fm waliokuwa wanaendesha kipindi cha Power breakfast kuhusishwa na kuacha kazi na Baadaye kutolewa taarifa na mmoja wa wakurugenzi wa Radio hiyo juu ya jambo hilo kuwa Mikataba yao imekwisha tarehe 31/3/2016 ndio mana hawakusikika katika kipindi hicho kwa siku ya leo Tarehe 1/4/2016 na kuwepo kwa Surprise ya watangazaji nguli waliokuwepo zamani akina Masoud Kipanya na Fina Mango.

Kufuatia Sakata hilo Mtangazaji Gerald Hando ameamua kuweka wazi kuhusiana na Jambo hilo kupitia akaunti yake ya Instagram na kuandika haya:

geraldhandoKwa Takribani Siku 3 Sasa Kumekuwa Na SINTOFAHAMU Na Kwa Baadhi Ya Ndugu Na Marafiki Imezua Taharuki Kuhusu Ajira Yangu Na Clouds FM..Naamiini Sasa Kwa Upande Wangu Ni Wakati MUAFAKA Kutoa TAMKO Rasmi Baada Ya kufuata Taratibu Zote Muhimu...KUANZIA LEO TAREHE 1 April 2016...Mimi Si Mfanyakazi Tena Wa Clouds Media Group Na Hii Ni Baada Ya Kwisha Rasmi Kwa Mkataba Wangu Na Clouds Media Group Jana 31 March 2016...Nimeamua Hivi Kwa HIARI Yangu Mwenyewe Bila SHINIKIZO Wala RABSHA Na Mwajiri Wangu Huyo Wa ZAMANI..Napenda Nikujulishe Tu Kuwa Nitaendelea Na Kazi Hii Hii Ya Utangazaji Ila Sasa Nitakua Na Kituo Kingine Na SI Clouds TENA...Wapi Na Lini Ni Suala La TIME...Jiandae Kuendelea Kufurahia ASUBUHI YAKO KATIKA FREQUENCY MPYA SOON. ..Haya Ni Masuala Ya FURSA...IKIJA UNAIKAMATA FASTA...Stay Cool...Stay Tuned😎😎😎!
 Gerald Hando

No comments:

Powered by Blogger.