Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam atoa siku 6, ombaomba Waondoke Jijini Dar es Salaam
SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa katika kuweka jiji hilo safi imejipanga kuanza na mambo matatu ambayo ni kuwaondoa ombaomba wa barabarani, kuwabana wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari na kuwaamuru wamiliki wa bar kutopiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ombaomba walikuja Dar es Salaam kwa nauli zao hivyo lazima warudi walikotoka kwa nauli zao.
Makonda ametoa siku sita mpaka April 18 ombaomba ndani ya jiji la Dar es salaam wawe wameondoka
Kuhusu wamiliki wa Bar, Makonda amesema wamiliki wa bar wanaowapigia watu kelele wafuate sheria walizopewa kama ni mwisho saa sita kupiga muziki iwe hivyo na muziki huo upigwe kwenye maeneo husika.
Amesema mtu ambaye anapiga muziki nje ya utaratibu wa kibali chake maana yake ajiandae kunyang’anywa leseni na kufutiwa kibali chake na faini hiyo atailipa mwenyewe.
Aidha, Makonda amewataka wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari walipe faini na kuweka utaratibu wa kupaki wapi magari yao au kubomoa majengo yao.
Aidha, Makonda amewataka wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari walipe faini na kuweka utaratibu wa kupaki wapi magari yao au kubomoa majengo yao.
No comments: