Lowassa: Siku za Magufuli zinahesabika
EDWARD Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania amesema kuwa, staili ya utawala wa Rais John Magufuli ni ya hamasa
na kwamba, atakuwa maarufu kwa kipindi kifupi, anaandika Faki Sosi.Akizungumza na wanzuoni kutoka ndani na nje ya nchi nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam jana Lowassa amesema, pamoja na hamasa anayofanya Rais Magufuli tangu aingie madarakani, haoni mafanikio ya uchumi wa taifa hili katika siku zijazo.
Mingoni mwa mambo ambayo Lowassa amesema yanamshangaza kwenye utawala wa Rais John Magufuli ni kuingilia hatua ya ugawaji fedha hivyo kupuuza chombo chenye mamlaka hayo ambacho ni bunge.
“Kazi ya rais si kugawa fedha, kazi hii hufanywa na bunge kwa kuwa ndio yenye mamlaka ya kuidhinisha bajeti,” amesema.
Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka jana kupitia Chadema na kuungwa mkono na Ukawa amewaeleza wanazuoni hao walioongozwa na Profesa Lwekeza Mukandala, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwamba, hatua ya utumbuaji majipu inayofanywa na Rais Magufuli kabla ya kujiridhisha ina kasoro.
“Nasononeshwa ninapoona wafanyakazi wa mashirika na taasisi za umma wanaachishwa kazi bila utaratibu,” amesema.
Kauli hii inafanana na ile aliyoitoa Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania hivi karibuni alipozungumza na MwanHALASI Online kuhusu utawala wa Rais Magufuli.
“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka,” Sheikh Ponda aliueleza mtandao huu.
Lowassa amesema kuwa, wakati Rais Magufuli akijinasibu kwamba anataka nchi ya viwanda, hali hio ni ngumu kufikiwa iwapo serikali yake itakosa ‘sapoti’ kutoka kwenye mataifa mengine ikiwemo Marekani.
Amesema hatua ya mataifa mbalimbali duniani kuisitishia misaada Tanzania ni pigo na maumivu makubwa katika uchumi wake.
“Wahisani si watu wa kuwabeza…, wanaweza kuturudisha nyuma, Jakaya (Rais Jakaya Kikwete) kwa kaisi fulani alijitahidi kidogo kuwavutia wawekezaji,” amesema.
Katika mazungumzo hayo Lowassa liwaambia wanazuoni hao kwamba, kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, upinzani ulishinda lakini Chama Cha Mainduzi (CCM) kilisaidiwa na vyombo vya dola.
No comments: