FULL STORY: Mkuu wa wilaya Richard Kasesela Alivyowapeleka Polisi Watangazaji Waliomuigiza Redioni siku ya Wajinga



Siku ya kwanza ya mwezi April kila mwaka huwa ni siku ya Wajinga duniani na kila mmoja anaeifahamu hii siku huwa anazishtukia baadhi ya habari na wengine huwa wanaifanyia mzaha kweli hii siku kama Watangazaji wa Redio E-bony FM Iringa ambao hawakuwa na nia mbaya kwa kilichotokea sema ndio wakajikuta Polisi baada ya Mkuu wa wilaya kuchukua hatua.

Boss wa Redio hiyo aitwae Edo Bashir aliiambia millardayo.com yafuatayo

‘Unajua ilikua siku ya Wajinga na vijana walichofanya ni ku-fake kama vyombo vya habari vingine vilivyofanya na nafikiri alivyoipokea Mheshimiwa ikawa tofauti, akawakamata na kuwatia ndani lakini nafikiri alielewa baadae ishu ikaisha‘
‘Walichofanya ni kuigiza sauti yake kwa kusema mkuu wa wilaya atakua sehemu flani kuwatembelea… sasa yeye akahisi  wametoa taarifa wakati yeye hakusema, haikuchukua muda Mkuu wa wilaya akawa ameshafika studio akiwa na Polisi‘ – Eddo
Kwenye mahojiano na millardayo.com Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema ‘nilikua nasikiliza Redio nikasikia mtu anahojiwa anajitangaza kwamba yeye ni mkuu wa wilaya na kujibu maswali na kutoa ahadi, walitangaza kuanzia jana yake kwamba mkuu wa wilaya atakuwepo, kitendo cha kutangaza jana yake tu yenyewe inaondoa ule usikukuu ya wajinga‘

‘Kisa cha mimi kuwaita wapelekwe Polisi ni ili waandike maelezo kiasi kwamba atakapotokea mtu yeyote atakaelalamika kwamba ilitokea ahadi ya mkuu wa wilaya tarehe moja haijatekelezwa au kuna kitu kimetokea, niwe na ushahidi wa kutosha kwamba wao ndio wamehusika kwahiyo wala sikuwaweka ndani, walikwenda tu kuandika maelezo zaidi‘ – Richard Kasesela
Kwenye sentensi nyingine Mkuu huyu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ambaye picha zake zimekua zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kumuonyesha jinsi anavyojitoa kwenye kazi za jamii amesema ‘Hawakukamatwa sababu sikukuu ya Wajinga siijui wala sielewi hapana…. nimewasamehe sababu hawakuelewa hilo ni kosa mi mwenyewe nilikwenda kuwatoa pale Polisi na kuongea nao wasirudie kutumia personality za watu au vyeo kuzungumza na jamii na ilichelewa sana kurekebishwa baada ya kupiga nyimbo tatu‘

Unataka kuipata hii stori kwa urefu na kuwasikia wahusika wote wakiiongelea? bonyeza play hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.