Cristiano Ronaldo anahamia PSG? Jibu liko hapa
staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real
Madrid
yaHispania Cristiano
Ronaldo kuhusishwa
kutaka kuhama Real Madrid na kutaka kujiunga na klabu ya Paris
Saint Germain ya Ufaransa zimerudi tena katika mitandao.
Awali Ronaldo aliwahi kuhusishwa kutaka kujiunga na PSG ila leo April 19 2016 stori kutoka
101greatgoals.com wameripoti kuwa Cristiano Ronaldo amewahi kukutana na Rais wa PSG Nasser
Al-Khelaifi mara
tano, stori zinaeleza kuwa Jose Mourinhohuenda
akajiunga na PSG pamoja na Ronaldo msimu ujao.
Taarifa za Ronaldo kukutana na Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi zimevuja
baada yaRonaldo kudaiwa
kuonekana akiwa Paris Ufaransa kwa ndege ya kukodi na kupelekwa
katika hoteli aliyopo Nasser
Al-Khelaifi na
siku inayofuatia Ronaldo anadaiwa kuondoka na ndege binafsi
tena kuwahi mazoezi ya Real Madrid.
Huenda kukawa kuna kitu kinaendelea kwani Ronaldo amekuwa akionekana Paris mara kadhaa sasa.
No comments: