BREAKING: Maamuzi ya mwisho kwenye kesi ya Mabula na Wenje yametangazwa leo


Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Nyamagana iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Nyamagana
 Ezekiah Wenje (CHADEMA) dhidi ya Mbunge wa sasa wa Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM) ilikuwa ikiendelea katika mahakama Kuu Mwanza ambapo Ezekiah Wenje alifungua kesi hiyo akipinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yakimpa ushindi Mbunge wa sasa, Stanslaus Mabula.
April 08 2016, maamuzi ya kesi hiyo yametangazwa ambapo Stanslaus Mabulaameshinda kesi hiyo, baada ya kuonekana upande wa madai hauna ushahidi unaokidhi, kuithibitishia mahakama. 

No comments:

Powered by Blogger.